143 Jina la Mungu Laweza Kuamuliwa na Viumbe?

1 Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na yanazidi uwezo wa mwanadamu kumjua Yeye. Lugha ya mwanadamu haina uwezo wa kumfafanua Mungu kwa ukamilifu. Mwanadamu ana msamiati finyu tu ambao anaweza kufafanua yote anayojua kuhusu tabia ya Mungu. Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu sana, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya?

2 Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe. Siku itawadia ambapo Mungu hataitwa Yehova, Yesu, au Masihi—Yeye Ataitwa tu Muumba. Wakati huo, majina yote ambayo Alichukua hapa duniani yatafikia kikomo, kwa kuwa kazi yake hapa duniani itakuwa imefika mwisho, na baada ya hapo Mungu hatakuwa na jina.

3 Wakati mambo yote yatakuja kuwa chini ya utawala wa Muumba, kwa nini umwite kwa jina sahihi ila bado halijakamilika? Je, bado unatafuta jina la Mungu sasa? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaitwa tu Yehova? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu? Je, unaweza kubeba dhambi ya kumkufuru Mungu? Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye atakuhitaji wewe, mmoja wa viumbe wake Wake, kuliamua?

Umetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 142 Unathubutu Kudai Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika Kamwe?

Inayofuata: 144 Umuhimu wa Jina la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp