982 Unaweza Kuokolewa Usipotelekeza Ukweli

Aya ya 1

Pasipo mtu kutazama matatizo yake inavyotakiwa,

itaathiri ufahamu wake kumhusu Mungu.

Wengine hugundua ubora wao wa tabia ni duni,

au dhambi kubwa hutekelezwa.

Kisha wanajikatia tamaa, wanapoteza matumaini,

wasitake kuteseka kwa sababu ya ukweli.

Hawatafuti kubadilisha tabia yao,

wakifikiri kuwa hawajawahi kubadilika.

Kiitikio

Hivi sasa, Nakuambia:

Wale wanaoshughulikia matatizo yao inavyotakiwa wana matumaini,

na watatoka kwenye hali zao hasi.

Jione kwa usahihi, usitelekeze ukweli.

Aya ya 2

Kwa kweli watu wengine wamebadilika,

lakini wao wenyewe hawaoni hilo kabisa.

Wao huangalia tu matatizo yao,

na kupoteza radhi ya kushirikiana na Mungu.

Hii itachelewesha kuingia kwao kwa kawaida,

itaongeza mawazo yao yasiyo sahihi kumhusu Mungu.

Zaidi ya hayo ina athari

katika hatima yao.

Kiitikio

Hivi sasa, Nakuambia:

Wale wanaoshughulikia matatizo yao inavyotakiwa wana matumaini,

na watatoka kwenye hali zao hasi.

Jione kwa usahihi, usitelekeze ukweli.

Aya ya 3

Wanapokuwa dhaifu, watafutaji wa ukweli bado hufanya wajibu

kwa uaminifu, bila kufikiria majaliwa yao.

Naona mabadiliko; na ukiangalia kwa makini,

utatambua kuwa sehemu ya upotovu wako imebadilika.

Lakini unapotumia viwango vya juu zaidi

kupima kukua kwako, licha ya kushindwa

kufikia viwango hivyo vya juu, pia utakana

mabadiliko ambayo umefanya—hilo ni kosa la kibinadamu.

Kiitikio

Hivi sasa, Nakuambia:

Wale wanaoshughulikia matatizo yao inavyotakiwa wana matumaini,

na watatoka kwenye hali zao hasi.

Jione kwa usahihi, usitelekeze ukweli.

Daraja

Ikiwa kwa kweli unaweza kutofautisha mema na mbaya,

basi chunguza mabadiliko yaliyomo ndani yako.

Licha ya kuona mabadiliko yako mwenyewe,

utapata njia ya kutendwa pia.

Utang’amua kwamba mradi utie bidii,

kuna tumaini la kuokolewa hata hivyo.

Kiitikio

Hivi sasa, Nakuambia:

Wale wanaoshughulikia matatizo yao inavyotakiwa wana matumaini,

na watatoka kwenye hali zao hasi.

Jione kwa usahihi, usitelekeze ukweli.

Umetoholewa kutoka katika katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 981 Mungu Awaokoa Wale Wanaopenda Ukweli

Inayofuata: 983 Mungu Awapenda Wale Walio na Azimio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki