728 Kweli Unaweza Kutii Utaratibu wa Mungu?

1 Je, mnayo nia ya kustarehe katika baraka Zangu duniani, baraka zilizo sawa na zile za mbinguni? Je, mko tayari kuchukua kuelewa kwao kunihusu, na kufurahia kwa maneno Yangu na ufahamu wako kunihusu, kama vitu vya thamani zaidi na vya muhimu zaidi katika maisha yenu? Je, kweli mnaweza kuwa watiifu Kwangu kikamilifu, bila fikira kwa matarajio yenu wenyewe? Je, kweli mna uwezo wa kujiruhusu kuuwawa na Mimi, na kuongozwa na Mimi, kama kondoo? Je, kunao kati yenu walio na uwezo wa kutimiza vitu kama hivi? Inawezekana kuwa wote wanaokubaliwa na Mimi na kupokea ahadi Zangu ndio wanaopokea baraka Zangu?

2 Je, mmeelewa chochote kutoka katika maneno haya? Nikiwajaribu, je, mnaweza kweli kujiweka wenyewe katika huruma Yangu, na, katikati ya majaribu haya, mtafute nia Yangu na muelewe moyo Wangu? Mimi sitamani wewe uweze kuongea maneno mengi matamu, au utoe hadithi nyingi za kufurahisha; badala yake Ninauliza kuwa uweze kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu, na kwamba unaweza kuingia kikamilifu na kwa kina katika hali halisi. Kama Singezungumza moja kwa moja, je, ungewacha kila kitu kilicho karibu na wewe na ukubali kutumiwa na Mimi? Je, hii siyo hali halisi Ninayohitaji? Je, ni nani aliye na uwezo wa kuelewa maana iliyo katika maneno Yangu?

3 Ilhali Ninauliza kuwa msishushwe na wasiwasi tena, kwamba mwe msitari ya mbele katika kuingia kwenu na muelewe kiini cha maneno Yangu. Hii itazuia hali ya nyinyi kutoelewa maneno Yangu, na hali ya kutokuwa na uwazi kuhusu maana Yangu, na hivyo kukiuka amri Zangu za utawala. Natumaini kuwa mtaelewa Nia Yangu kwenu katika maneno Yangu. Msifikiri juu ya matarajio yenu tena, na mtende vile ambavyo mmeamua mbele Yangu kutii mipango ya Mungu katika kila kitu. Wale wote wanaosimama miongoni mwa kaya Yangu wanapaswa kufanya mengi kiasi wanachoweza; unafaa utoe hali yako bora zaidi kwa sehemu ya mwisho ya kazi Yangu duniani. Je, unayo nia ya kuviweka vitu vya aina hii katika matendo?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 4” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 727 Viumbe Walioumbwa Wanapaswa Kumtii Muumba

Inayofuata: 730 Jinsi ya Kutii Mamlaka ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp