541 Fuata Maneno ya Mungu ili Kutupilia Mbali Ushawishi Mbaya

1 Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kufuatilia ukweli—ni hapo tu ndipo utakuwa na hali sahihi. Kuishi katika hali sahihi ndilo sharti la mwanzo la kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali sahihi ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli. Basi, kuepuka ushawishi wa giza hakutawezekana. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza.

2 Kuishi katika hali sahihi ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika uhalisi wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu.

3 Wale ambao wameepuka ushawishi wa giza wataweza kufahamu mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, wataelewa mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, na hatimaye kuwa wasiri wa Mungu. Hawatakosa dhana kumhusu Mungu tu, na kukosa uasi dhidi Yake, lakini watakuja kuchukia hata zaidi dhana na uasi ambao walikuwa nao kabla, kusababisha upendo wa kweli kwa Mungu mioyoni mwao. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, naye humhitaji mtu amilikiwe na maneno Yake na upendo wa mtu Kwake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anapaswa kutafuta kutoka ndani ya maneno Yake, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno Yake, kukimbiakimbia kwa ajili ya maneno ya Mungu, kuishi kwa ajili ya maneno ya Mungu—haya yote ni mambo ambayo mtu anapaswa kufikia.

Umetoholewa kutoka katika “Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 540 Tupilia Mbali Ushawishi wa Giza ili Upatwe na Mungu

Inayofuata: 542 Ukweli wa Leo Unapewa Wale Wanaoutamani na Kuutafuta

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp