707 Mabadiliko Katika Tabia Hayatengani na Maisha Halisi

1 Katika kumwamini Mungu, iwapo mwanadamu anataka mabadiliko kwa tabia yake mwenyewe, basi lazima asijitenge na maisha halisi. Katika maisha halisi, lazima ujijue mwenyewe, ujitelekeze mwenyewe, utende ukweli, na vilevile kujifunza kanuni, maarifa ya kawaida na masharti ya kujiendesha katika mambo yote kabla ya wewe kuweza kutimiza mabadiliko ya polepole. Iwapo utalenga tu ujuzi katika nadharia na kuishi tu katika sherehe za dini bila ya kuingia ndani ya uhalisi, bila kuingia kwenye maisha halisi, basi hutaweza kamwe kuingia katika uhalisi, hutaweza kujijua mwenyewe, kuujua ukweli, au kumjua Mungu, na utakuwa kipofu na mjinga milele.

2 Wale wanaomkaidi Mungu wote ni watu ambao hawawezi kuingia katika maisha halisi. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ubinadamu lakini wanaishi kwa kudhihirisha asili ya pepo mbaya. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ukweli lakini wanaishi kwa kudhihirisha kanuni badala yake. Wale wasioweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi ni wale wanaoamini katika Mungu lakini wanachukiwa na kukataliwa na Yeye. Lazima ufanye mazoezi ya kuingia kwako katika maisha halisi, ujue upungufu wako mwenyewe, ukaidi na upumbavu, na ujue ubinadamu wako usio wa kawaida na udhaifu. Kwa njia hiyo, ufahamu wako wote utaambatanishwa ndani ya hali yako halisi na ugumu. Ni aina hii ya ufahamu pekee ndiyo ya kweli na inaweza kukufanya ushike kwa hakika hali yako mwenyewe na ufanikishe mabadiliko ya tabia yako.

Umetoholewa kutoka katika “Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 706 Jinsi Mungu Apimavyo Mabadiliko Katika Tabia za Watu

Inayofuata: 708 Mchakato wa Badiliko Katika Tabia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp