304 Kuja kwa Mwana wa Adamu Kunawafunua Watu Wote

1 Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao huenda hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote.

2 Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa “kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani” na “kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake.” Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi?

3 Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia, na akili yako isiyotii na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama Yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi.

4 Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?

Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 303 Una Imani ya Kweli Katika Kristo?

Inayofuata: 305 Hustahili Kuwasiliana na Mungu kwa Mantiki kama Hiyo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp