959 Matokeo ya Kukera Tabia ya Mungu

1 Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga, au hata wale wanaomkashifu—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mwelekeo wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mwelekeo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao.

2 Mungu hutumia ujio wa hoja katika kushughulikia tabia yenye uovu ya baadhi ya watu. Wakati hoja hizi zinapofanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia ya uovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuona ya kuadhibiwa au kuuawa.

3 Hivyo basi wakati watu wanapompinga Mungu, na kumkashifu na kumkufuru Yeye, kama wataendelea kusema ubaya kuhusu tabia Yake, au kama watafikia ile hali ya kimsingi ya Mungu, athari zake hazifikiriki. Athari zile mbaya zaidi ni kwamba Mungu anayakabidhi maisha yao na kila kitu chao kwa Shetani, mara moja na kabisa. Hawatasamehewa daima dawamu. Hii inamaanisha kwamba mtu huyu amekuwa chakula katika kinywa cha Shetani, mwanasesere katika mikono yake, na kuanzia hapo, Mungu hahusiki naye.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 958 Kanuni za Mungu za Kutenda Hazibadiliki

Inayofuata: 960 Jinsi ya Kutoikosea Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp