806 Matokeo ya Kutojua Tabia ya Mungu

1 Kama huelewi tabia ya Mungu, basi haitawezekana kwako kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, haitawezekana wewe kumwonyesha heshima na uchaji, lakini badala yake utakuwa tu mzembe asiyejali na kuepuka kusema ukweli wote, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Ingawa kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakini au kudadisi masuala haya. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuzilia mbali amri za utawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na tunda la msingi la tendo lako linakuwa ni kosa dhidi ya amri ya utawala.

2 Kwamba Ninawaomba muelewe tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkikosea amri za utawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, basi kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba, pamoja na kuchunguza mienendo yenu binafsi, muwe waangalifu zaidi na hatua mnazochukua. Haya ndiyo yatakuwa mahitaji ya juu zaidi nitakayowaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtayafikiria kwa umakini na kuyaona kuwa muhimu kabisa. Endapo siku ifike ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakutakuwa na mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 805 Ni Wale tu Wanaomjua Mungu Ndio Wanaweza Kumshuhudia

Inayofuata: 807 Unapaswa Kumwiga Petro

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp