243 Matokeo ya Kumkataa Kristo wa Siku za Mwisho

1 Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu?

2 Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 242 Kumkataa Kristo wa Siku za Mwisho ni Kumkufuru Roho Mtakatifu

Inayofuata: 244 Kumwasi Mungu Kunaweza Kuishia tu kwa Adhabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp