723 Vigezo vya Utiifu wa Mwanadamu kwa Mungu

1 Katika kupima ikiwa watu wanaweza kumtii Mungu au la, jambo muhimu la kuangalia ni ikiwa wanatamani kitu chochote cha kupita kiasi kutoka kwa Mungu, na ikiwa wana nia mbaya au la. Ikiwa watu humdai Mungu kila wakati, inathibitisha kuwa wao sio watiifu Kwake. Ukimdai Mungu, hii inathibitisha kwamba unafanya maafikiano na Mungu, kwamba unachagua mawazo yako mwenyewe, na kutenda kulingana na mawazo yako mwenyewe. Kwa kufanya hivi, unamsaliti Mungu, na huna utiifu. Hakuna maana katika kumdai Mungu; ikiwa unaamini kweli kwamba Yeye ni Mungu, basi hutathubutu kumdai, wala hutastahiki kumdai, yawe madai ya maana au la. Ikiwa una imani ya kweli, na unaamini kuwa Yeye ni Mungu, basi hutakuwa na budi ila kumwabudu na kumtii.

2 Siku hizi, sio tu kuwa watu wana chaguo, lakini hata wanadai kwamba Mungu atende kwa mujibu wa mawazo yao wenyewe, wanachagua mawazo yao wenyewe na wanataka Mungu atende kulingana nayo, na hawahitaji wao wenyewe kutenda kulingana na kusudi la Mungu. Kwa hivyo, hakuna imani ya kweli ndani yao, wala kiini ambacho kimo ndani ya imani hii. Ikiwa unaweza kutii kwa kweli, basi utaweza kumfuata kwa moyo na akili moja bila kujali kama Anakutumia au la, utaweza kutumia rasilmali kwa ajili Yake, bila kujali kama una hadhi. Ni wakati huo tu ndipo utakapokuwa na akili, na kuwa mtu anayemtii Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 722 Mtii Mungu Mwenye Mwili ili Ukamilishwe

Inayofuata: 724 Cha Muhimu Katika Kumtii Mungu ni Kukubali Nuru Mpya Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp