689 Kupitia Upogoaji na Ushughulikiwaji ni kwa Maana Sana

1 Watu wengine wanakuwa wa kutoonyesha hisia baada ya kupogolewa na kushughulikiwa; wanapoteza nguvu zote kutekeleza wajibu wao, na wanaishia kupoteza uaminifu wao vile vile. Kwa nini hivi? Kwa kiasi ni kwa ajili ya kukosa kwao ufahamu kuhusu kiini cha matendo yao, na hili husababisha wao kutoweza kutii kupogolewa na kushughulikiwa. Pia kwa kiasi ni kwa ajili ya kutoweza kwao bado kuelewa umuhimu wa kupogolewa na kushughulikiwa ni upi. Watu wote huamini kwamba kupogolewa na kushughulikiwa kunamaanisha kwama matokeo yao yameamuliwa tayari. Kwa sababu hiyo, wao huamini kimakosa kuwa wakiwa na uaminifu kiasi kwa Mungu, basi hawafai kushughulikiwa na kupogolewa; na wakishughulikiwa, basi hili haliashirii upendo na Haki ya Mungu. Suitafahamu kama hiyo huwasababisha watu wengi kutothubutu kuwa “waaminifu” kwa Mungu. Kwa kweli, baada ya yote, ni kwa sababu ni waongo kupindukia; hawataki kupitia ugumu. Wanataka tu kupata baraka kwa njia rahisi.

2 Watu hawana ufahamu wa haki ya Mungu. Si kwamba Hajafanya lolote la haki au kwamba Hafanyi chochote cha haki; ni tu kwamba watu daima hawaamini kwamba kile Afanyacho Mungu ni haki. Machoni pa wanadamu, kama kazi ya Mungu haipatani na matamanio yao ya kibinadamu, ama kama hailingani na matarajio yao, basi lazima Yeye si mwenye haki. Hata hivyo, watu kamwe hawajui kwamba matendo yao ni yasiyofaa na kwamba hayaambatani na ukweli, wala hawatambui kamwe kwamba matendo yao yanampinga Mungu. Kama Mungu hangewashughulikia ama kuwapogoa watu kwa ajili ya dhambi zao na wala kuwakaripia kwa sababu ya makosa yao, lakini daima angekuwa mtulivu, kamwe bila kuwakasirisha, daima bila kuwakosea, na daima bila kufunua makovu yao, lakini angewakubalia kula na kuwa na wakati mzuri na Yeye, basi watu hawangelalamika kuwa Mungu sio mwenye haki. Wangesema kuwa Mungu ni mwenye haki kwa unafiki.

3 Kwa hivyo, watu bado hawaamini kuwa kile ambacho Mungu Anahitaji ni utendaji wao baada ya kubadilishwa kwao. Je, Mungu angekuwa vipi na uhakika kama wangeendelea na hayo? Kama Mungu angewasuta watu kidogo, hawangeamini tena kuwa Yeye huona utendaji wao baada ya mabadiliko. Wangeacha kuamini kuwa Yeye ni mwenye haki, na hawangekuwa na radhi kubadilishwa. Kama watu wangeendelea na hali hii, wangehadaiwa na mawazo yao wenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Maana Ndani ya Mungu Kuamua Matokeo ya Watu Kupitia Utendaji Wao” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 688 Bila Kujali Afanyayo Mungu, Yote ni kwa Ajili ya Kuwaokoa Binadamu

Inayofuata: 690 Lazima Utafute Mapenzi ya Mungu Ugonjwa Unapotokea

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp