620 Toa Moyo Wako kwa Kuyatenda Mapenzi ya Mungu

1 Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. Unapaswa daima kuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu, na uwe na tabia thabiti. Kuwaza kwako lazima kuwe kwa busara na wazi na hakupaswi kuyumbishwa au kudhibitiwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Unapaswa kuwa mtulivu daima katika uwepo wangu na daima udumishe ukaribu wa kuendelea na kushiriki na Mimi. Ni sharti uonyeshe nguvu na ukakamavu na usimame imara katika ushahidi wako Kwangu. Simama na kuzungumza kwa ajili Yangu na usiogope kile ambacho watu wengine wanasema. Zingatia kukidhi nia Zangu na usidhibitiwe na wengine. Kile Ninachokufichulia lazima kifanywe kwa mujibu wa nia Zangu na hakiwezi kucheleweshwa.

2 Mimi ni msaada wako na kinga yako, na vyote viko mikononi Mwangu, hivyo unaogopa nini? Je, huko sio kuwa na mhemuko sana? Lazima utupilie kando hisia haraka sana; Sitendi kwa kufuata muhemko, bali Ninatenda haki badala yake. Kuwa na imani! Kuwa na imani! Mimi ni mwenyezi wako. Hiki ni kitu ambacho unaweza ukakitambua kiasi, lakini bado unapaswa kutahadhari. Kwa ajili ya kanisa, mapenzi Yangu, na usimamizi Wangu, lazima ujitoe kikamilifu, na siri zote na miisho yote itaonyeshwa kwako. Hakutakuwa na uchelewaji zaidi na siku zitafikia mwisho. Kwa hiyo utafanya nini? Unawezaje kutafuta kuyafanya maisha yako yakomae kwa kasi zaidi? Je! Utafanyika mwenye manufaa Kwangu haraka kiasi gani? Utafanyaje ili mapenzi Yangu yatekelezwe? Ili kufanya hivyo kunahitaji kutafakari kikamili na ushirika wa kina zaidi na Mimi. Nitegemee Mimi, niamini Mimi, usiwe mzembe kamwe, na uweze kufanya mambo kulingana na mwongozo Wangu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 9” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 619 Pigana Mapigano Mazuri kwa Ajili ya Ukweli

Inayofuata: 621 Mtu Hawezi Kumhudumia Mungu Asipobadilisha Tabia Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp