705 Mabadiliko ya Tabia Pekee Ndiyo Mabadiliko ya Kweli

1 Kubadilisha tabia ya mwanadamu huanza na maarifa ya kiini chake na kupitia mabadiliko katika mawazo yake, asili, na mtazamo wa akili—kwa njia ya mabadiliko ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndio mabadiliko ya kweli yatapatikana katika tabia ya mwanadamu. Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili, kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli.

2 Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. Kama hisia ya mwanadamu na utambuzi hauwezi kubadilika, basi mabadiliko katika tabia yake hayawezekani, sawa na kuwa baada ya moyo wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 704 Kuijua Asili Yako Mwenyewe ni Muhimu kwa Badiliko Katika Tabia

Inayofuata: 706 Jinsi Mungu Apimavyo Mabadiliko Katika Tabia za Watu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp