761 Una Upendo wa Kweli kwa Mungu?

1 Kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa?

2 Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika wakati wa kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa kufungwa na kupumbazwa na Shetani.

3 Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa. Je, uko tayari kuwa mtu wa aina hii? Je, uko tayari kukubaliwa na Mungu? Je, uko tayari kutoroka kutoka miliki ya Shetani na kurudi kwa Mungu? Je, sasa wewe ni mali ya Shetani au umehesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme?

Umetoholewa kutoka katika “Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 760 Upendo Safi Bila Dosari

Inayofuata: 762 Humpendi Mungu Kwa Dhati

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp