292 Watu Hawajui Wokovu wa Mungu

1 Madhumuni na umuhimu wa kuwasili Kwangu miongoni mwa mwanadamu ni kuwaokoa wanadamu wote, kuwaleta watu wote katika nyumba Yangu, kuunganisha mbingu pamoja na ardhi, na kufanya mwanadamu kufikisha “ishara” kati ya mbingu na dunia, kwa maana hiyo ndiyo kazi asili ya mwanadamu. Wakati Nilimuumba mwanadamu, Nilifanya mambo yote yawe tayari kwa ajili ya mwanadamu, na baadaye, Mimi Nikamruhusu mwanadamu kupokea utajiri Niliompa kulingana na masharti Yangu. Ndio maana Nasema ni kwa uongozi Wangu ndio maana wanadamu wote wamefikia siku hii. Na haya yote ni Mpango Wangu.

2 Miongoni mwa watu wote, idadi kubwa ya watu ipo chini ya ulinzi wa Upendo Wangu, na idadi kubwa inaishi chini ya kuadibu kwa chuki Yangu. Ingawa watu wote wanaomba Kwangu, bado hawana uwezo wa kubadili hali yao ya sasa; mara tu wamepoteza matumaini, wanaweza tu kuwacha hali asili ichukue mkondo wake na kusitisha uasi Kwangu, kwa maana haya ndiyo yote yanayoweza kukamilishwa na mwanadamu. Inapokuja kwa hali ya maisha ya mwanadamu, mwanadamu bado hajapata maisha halisi, yeye bado hajaona kupita katika udhalimu, ukiwa, na hali duni ya dunia—na hivyo, kama haingekuwa ujio wa maafa, watu wengi bado wangekumbatia hali halisi ya dunia, na bado wangejishughulisha katika ladha ya “uzima.” Je, hii si hali halisi ya dunia? Je, hii si sauti ya wokovu Ninayonena kwa mwanadamu?

3 Kwa nini, miongoni mwa wanadamu, hakuna kamwe aliyenipenda kwa kweli? Ni kwa nini mwanadamu ananipenda tu katikati ya kuadibu na majaribu, lakini hakuna mwanadamu Anayenipenda chini ya ulinzi Wangu? Mimi Nimetoa kuadibu Kwangu mara nyingi juu ya mwanadamu. Wao wanaiangalia, kisha wanaipuuza, na hawawezi kujifunza na kutafakari juu yake kwa wakati huu, na hivyo yote yanayokuja juu ya mwanadamu ni hukumu isiyo na huruma. Hii ni mojawapo tu ya mbinu Zangu za kazi, lakini bado ni kwa ajili ya kumbadili mwanadamu na kumfanya aweze kunipenda.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 29” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 291 Nani Awezaye Kumjua Mungu Ajapo?

Inayofuata: 293 Mungu Anatarajia Kuwa Binadamu Wataweza Kuendelea Kuishi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp