532 Wasioyatenda Maneno ya Mungu Wataondolewa

1 Kazi na neno la Mungu vinanuiwa kusababisha badiliko katika tabia yenu; lengo Lake si tu kuwafanya muelewe ama mjue kazi na neno Lake. Hilo halitoshi. Wewe ni mtu aliye na uwezo wa kufahamu, kwa hivyo hupaswi kuona ugumu kuelewa neno la Mungu, kwa sababu maneno mengi ya Mungu yameandikwa katika lugha ya mwanadamu, na Anazungumza kwa uwazi sana. Unaweza kabisa kujifunza ni nini ambacho Mungu angetaka uelewe na utende; hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida aliye na uwezo wa kufahamu anapaswa kuweza kufanya.

2 Maneno ambayo Mungu anasema katika hatua ya sasa ni ya wazi na dhahiri zaidi, na Mungu anaonyesha mambo mengi ambayo watu hawajayazingatia, na vilvile kila aina ya hali za binadamu. Maneno Yake yanajumuisha yote na ni dhahiri kama mwanga wa mwezi kamili. Kwa hivyo sasa, watu wanaelewa masuala mengi, lakini bado kuna kitu kinachokosa—watu kuweka neno Lake katika vitendo. Ni lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa utondoti, na wauchunguze na kuutafuta kwa kina zaidi, badala ya kusubiri tu kufyonza chochote wanachopewa; vinginevyo wanakuwa kupe tu. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hapendi ukweli na mwishowe ataondolewa.

Umetoholewa kutoka katika “Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 531 Mwanadamu ni Mgumu Sana Kuokoa

Inayofuata: 533 Yeyote Asiyetenda Ukweli Ataondolewa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp