536 Wasiofuatilia Ukweli Hawawezi Kufuata Hadi Mwisho

Kazi ambayo Mungu Anaitekeleza katika watu ni kimsingi kuwawezesha kuupata ukweli; Kukufanya wewe kufuatilia maisha ni kwa ajili ya kukukamilisha, na yote ni ya kukufanya ufae kutumika na Mungu. Yote unayofuata sasa ni kusikia siri, kusikiliza maneno ya Mungu, kulisha macho yako, kuona kitu kipya ama kuona ni mwenendo upi, na kuridhisha udadisi wako. Kama hii ndio nia ya moyo wako, hakuna vile utafikia mahitaji ya Mungu. Wale ambao hawafuati ukweli hawezi kufuata mpaka mwisho kabisa. Wakati huu, si kwamba Mungu hafanyi kitu—ni kwamba watu hawashirikiani, kwa sababu wamechoka na kazi Yake. Wanataka tu kusikia maneno ya baraka Yake, na hawataki kusikia maneno ya hukumu Yake na kuadibiwa. Sababu ya hii ni nini? Ni kwa sababu tamaa ya watu kupata baraka haijatimizwa, na wako hasi na wanyonge. Si kwamba Mungu kimakusudi hakubali watu kumfuata, na si kwamba anapeana mapigo kimakusudi kwa wanadamu. Watu wako hasi na wanyonge kwa sababu nia zao hazifai. Mungu ni Mungu Ambaye Anampa mwanadamu maisha, naye hawezi kumleta mwanadamu katika kifo. Uhasi wa watu, unyonge na kurudi nyuma yote yanasababishwa na wao wenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 535 Wale Wasiofuatilia Ukweli Watajuta

Inayofuata: 537 Kuelewa Ukweli Ukaribiapo Kufa Kumechelewa Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp