572 Wale Wanaoshuku na Kukisia Kuhusu Mungu ni Wadanganyifu Zaidi

1 Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.

2 Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogondogo, anayependelea na asiye na mantiki, aliyekosa hisia ya haki, mwenye mbinu ovu, mdanganyifu na mjanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya kwamba hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasio na ujuzi huu hawatakaribishwa na watapoteza nafasi yao katika nyumba ya Mungu.

3 Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli?

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 571 Kukubali Ukweli Ndiyo Njia ya Pekee ya Wokovu

Inayofuata: 573 Wajibu wa Mtu ni Wito wa Kiumbe Aliyeumbwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp