310 Una Vipengele Vingi vya Kutomwamini Kristo

1 Kwa wakati huu, kuna kutoamini kwingi sana ndani yenu. Jaribu kuangalia kwa makini ndani yako na kwa hakika mtajionea jibu mwenyewe. Unapopata jibu halisi, basi utakubali kuwa wewe kweli si muumini wa Mungu, bali ni mdanganyifu, unayekufuru, unayemsaliti, na usiye mwaminifu kwa Mungu. Kisha utagundua kuwa Kristo si mwanadamu, ila ni Mungu. Siku hiyo itakapowadia, basi utamheshimu, utamcha na utampenda kwa dhati Kristo.

2 Kwa sasa, imani yenu ni asilimia thelathini tu ya moyo wenu, ilhali asilimia sabini zimekumbwa na shaka. Tendo lolote likifanywa na sentensi yoyote ikitamkwa na Kristo vyaweza kusababisha muwe na fikira na maoni kumhusu Yeye. Fikira na maoni haya hutokana na kutokuwa na imani kabisa ndani Yake. Mnamtamani na kumcha tu Mungu msiyemwona aliye mbinguni lakini hauna haja na Kristo Anayeishi duniani. Hii pia si ni ukosefu wa imani? Mnamtamani tu Mungu Aliyefanya kazi kitambo kile lakini hutaki kukumbana na Kristo wa leo. Hizi ndizo huwa “imani” zilizochanganyika katika mioyo yenu isiyomwamini Kristo wa leo.

3 Sikuchukulii kwa hali ya chini kwa maana ndani yako mna kutoamini kwingi, ndani yenu mna uchafu mwingi sana ambao lazima uchunguzwe kwa kina. Madoa na uchafu huu ni ishara kuwa huna imani hata kidogo; ni alama za ninyi kumkana Kristo na huonyesha kuwa nyinyi ni msaliti wa Kristo. Hiyo ni kama kitambaa kinachofunika ufahamu wenu wa Kristo, kizuizi cha nyinyi kupatwa na Kristo, kitu kinachowakinga kulingana na Kristo, na dhihirisho kuwa Kristo Hawatambui. Huu ndio wakati wa kuchunguza kila sehemu ya maisha yenu! Kufanya hivyo kutakufaidi kwa njia zote ambazo mnaweza kufikiria!

Umetoholewa kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 309 Una Imani na Upendo wa Kweli kwa Kristo?

Inayofuata: 311 Mwanadamu Hana Imani ya Kweli Katika Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp