Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

282 Iga Uzoefu wa Petro

1 Baada ya Petro kupitia kiasi fulani cha kazi ya Mungu, alipata umaizi kiasi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia.

2 Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu. Wakati mwingine bado alikuwa na upinzani na uasi. Baada ya Yesu kutundikwa msalabani, hatimaye alizinduka kidogo na alihisi kuwa mwenye kustahili adhabu. Hatimaye ilifikia hatua ambapo hakuwa anakubali wazo lolote alilokuwa nalo ambalo halikuwa sahihi.

3 Alijua hali yake mwenyewe vizuri sana, na pia alijua utakatifu wa Bwana vizuri. Matokeo yake ni kwamba, moyo wa upendo kwa Bwana ulikua ndani yake hata zaidi, na alilenga katika maisha yake zaidi. Kwa sababu ya hiyo alipitia dhiki kubwa, na ingawa wakati mwingine ilikuwa kama kwamba alikuwa na ugonjwa mkubwa na hata alionekana kuchungulia kaburi, baada ya kusafishwa kwa njia hii mara nyingi, alikuwa na ufahamu zaidi wa nafsi yake, na kwa njia hii tu ndipo alipata upendo wa kweli kwa Bwana.

4 Inaweza kusemwa kuwa maisha yake yote yaliishiwa katika usafishaji, na hata zaidi, yaliishiwa katika kuadibiwa. Uzoefu wake ulikuwa tofauti na wa mtu mwingine yeyote, na upendo wake ulizidi ule wa mtu yeyote ambaye hajakamilishwa. Sababu yake kuchaguliwa kama mfano ni kwamba alipitia uchungu mwingi sana maishani mwake na uzoefu wake ulikuwa wenye mafanikio mengi sana. Ikiwa kweli mnaweza kutembea hatua ya mwisho ya njia kama vile Petro, basi hakuna kiumbe hata mmoja ambaye anaweza kuchukua baraka zenu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Maisha ya Maana Zaidi

Inayofuata:Mwache Mungu Aingie Moyoni Mwako

Maudhui Yanayohusiana

 • Furaha Katika Nchi ya Kanaani

  1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu kuingia kati…

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…