242 Nimefurahia Upendo Mwingi wa Mungu

1 Mimi ni mtu mpotovu aliyejaa tabia ya kishetani. Hukumu na ufunuo wa maneno hunifanya nihisi nimeaibika. Nimeona upotovu wangu ni wa kina sana, nina mfano mdogo sana wa binadamu. Na sina uhalisi wowote wa ukweli. Hili linauhuzunisha moyo wangu. Kwa kimya nalia kwa dhiki. Kwa nini siwezi kukuridhisha? Nikiona jinsi Unavyosubiri kutubu kwangu kwa dukuduku, sipotei na kukata tamaa tena. Upendo Wako unauvunja moyo wangu, upendo Wako unafanya machozi yangu yatiririke kama mvua. Upendo Wako umeushinda moyo wangu, umenifanya nikupende zaidi sana. Nimepata ukweli kwa kukufuata, ni Wewe tu Uliye mzuri sana.

2 Kwa kupitia hukumu ya maneno Yako, nimeona vizuri ukweli wa upotovu Wangu. Sina ubinadamu wala busara, lakini bado nina kiburi na mwenye kujidai. Ninachoishi kwa kudhihirisha yote ni tabia ya kishetani, ilhali nafikiri nina ubinadamu mzuri. Nimeona upotovu wangu ni wa kina sana na nahitaji utakaso na wokovu Wako. Kila neno la hukumu Yako linafunua chanzo cha upotovu wangu. Natubu na kusujudu, nimeona haki Yako. Binadamu wapotovu kupata hukumu na utakaso ni upendo Wako tu. Kuishi mbele Yako leo ni wokovu Wako kabisa. Ninapata neema ya wokovu Wako, upendo wangu Kwako unakuwa safi.

3 Naweza kuwa katika jaribio, lakini moyo wangu unahisi upendo Wako. Kupitia usafishaji, maneno Yako ni faraja yangu, najua Unanikamilisha. Kupokea utakaso na wokovu Wako kweli ni neema Yako. Nimeona upendo mkubwa uliojificha ndani ya hukumu na kuadibu Kwako. Nahisi furaha kwamba naweza kukupenda, siwezi kuzuia sifa zangu Kwako. Upendo Wako ni mkubwa sana, wa kweli sana, mzuri sana, furaha yangu haiishi. Moyo wangu ni Wako kabisa, siku zote nitakuinua na kukushuhudia. Ningependa kukupenda siku zangu zote, kwa Wewe kupata upendo wangu. Umenipa upendo mwingi sana, ningependa kukupenda milele.

Iliyotangulia: 241 Upendo wa Mungu Daima Unabaki Moyoni Mwangu

Inayofuata: 243 Moyo Wangu Hauhitaji Chochote Kingine

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp