Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

1034 Kiini cha Kristo ni Upendo

Ni nini kiini cha Kristo? Kwa wanadamu, kiini cha Kristo ni upendo; kwa wale wanaomfuata, ni upendo usio na mpaka. Kama Hangekuwa na upendo au huruma, basi watu wasingekuwa bado wanammfuata.

1 Katika kazi Mungu Anayofanyia binadamu wakati ambapo Yeye ni mwenye mwili, kiini Chake dhahiri na maarufu zaidi ni upendo; ni stahamala isiyo na mwisho. Ikiwa kiini Chake hakingekuwa upendo, ila badala yake kiwe jinsi mnavyofikiria—kwamba Mungu angeweza kumpiga yeyote Atakaye na kuadhibu, laani, hukumu, na kuadibu yeyote Achukiaye—basi Angekuwa mkali sana! Mnafikiri kwamba wakati wowote Yeye anakasirishwa na watu, watatetemeka kwa hofu na kutoweza kusimama mbele zake… Hii ni njia moja tu ambayo kwayo tabia ya Mungu huonyeshwa. Mwishowe, azma Yake bado ni wokovu. Upendo Wake unadhihirika kupitia ufichuzi wote wa tabia Yake.

2 Wakati wa kufanya kazi katika mwili, jambo ambalo Mungu hufichua zaidi kwa watu ni upendo. Uvumilivu ni nini? Uvumilivu ni kuwa na huruma kwa sababu ya upendo ndani, na azma Yake bado ni kuwaokoa watu. Mungu anaweza kuwa na huruma juu ya watu kwa sababu Yeye Ana upendo. Kama Mungu angekuwa tu na chuki na hasira, na kutoa tu hukumu na kuadibu, bila upendo wowote ndani ya hayo, basi hali isingekuwa muonavyo sasa na maafa yangewafikia nyinyi watu. Je, Angeweza kuwapa ukweli? Mngekuwa mmelaaniwa baada ya kurudi na kuhukumiwa, na kisha mngepitia msiba mkubwa. Basi wanadamu wa leo wangewezaje kuwepo bado?

3 Chuki ya Mungu, ghadhabu, na haki yameonyeshwa yote kwa msingi wa kuokoa kundi hili la watu. Upendo na huruma pamoja na subira kubwa mno pia yako ndani ya tabia hizi. Hii chuki ina hisia ya kutokuwa na chaguo lingine, ni kwa pamoja na shaka isiyokuwa na mpaka na kutazamia kwa binadamu! Chuki ya Mungu imelengwa kwa upotovu wa binadamu, imelengwa ukaidi wa binadamu na dhambi; ni ya upande mmoja, na imeimarishwa juu ya msingi wa upendo. Ni wakati tu kuna upendo ndipo chuki huwepo. Chuki ya Mungu kuelekea kwa binadamu ni tofauti na chuki Yake kuelekea kwa Shetani, kwa sababu Mungu anaokoa watu, na Yeye hamwokoi Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia:Mungu Ampenda Mwanadamu na Majeraha

Inayofuata:Kila Kitu Ambacho Mungu Humfanyia Mwanadamu Ni Cha Kweli

Maudhui Yanayohusiana

 • Tilia Maanani Majaliwa ya Binadamu

  1 Mungu anawahimiza watu wa makabila yote, nchi zote na hata nyanja: Sikilizeni sauti ya Mungu na kuona kazi Yake; tilia maanani jaala ya binadamu; mf…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …