441 Jinsi ya Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida Na Mungu

1 Kuanzishwa kwa uhusiano wa kawaida na Mungu kunaweza kufikiwa kabisa kwa moyo ulio kimya katika uwepo wa Mungu. Kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu kunamaanisha kuweza kutokuwa na shaka na kutoikana kazi yoyote Yake na kuweza kuitii kazi Yake. Kunamaanisha kuwa na nia zisizo na makosa katika uwepo wa Mungu, kutofanya mipango kwa ajili yako mwenyewe, na kuzingatia masilahi ya familia ya Mungu kwanza katika mambo yote; kunamaanisha kukubali uchunguzi wa Mungu na kuitii mipango ya Mungu. Lazima uweze kuutuliza moyo wako katika uwepo wa Mungu katika yote ufanyayo. Hata kama huyaelewi mapenzi ya Mungu, bado unapaswa kutekeleza wajibu na majukumu yako kadiri uwezavyo. Mara tu mapenzi ya Mungu yanapofichuliwa kwako, lichukulie hatua, na hutakuwa umechelewa mno.

2 Wakati ambapo uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa kwa msingi wa maneno ya Mungu. Kula na unywe maneno ya Mungu, kisha uyatie matakwa ya Mungu katika vitendo, rekebisha maoni yako, na uepuke kufanya chochote ili kumpinga Mungu au kulivuruga kanisa. Usifanye chochote ambacho hakifaidi maisha ya ndugu zako, usiseme chochote kisichowasidia wengine, na usifanye jambo lolote la aibu. Kuwa mwenye haki na mwenye heshima katika jambo unalotenda na uhakikishe kuwa kila kitendo chako kinapendeza mbele za Mungu. Ingawa wakati mwingine mwili unaweza kuwa dhaifu, lazima uweze kuweka masilahi ya familia ya Mungu kwanza, bila tamaa ya kupata faida ya kibinafsi, na lazima uweze kutenda kwa haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa namna hii, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Umetoholewa kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 440 Maisha Ya Kiroho Yanayofaa Yanapaswa Kudumishwa Daima

Inayofuata: 442 Ni Muhimu Kuwa na Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp