764 Kumpenda Mungu, Lazima Upitie Uzuri Wake

1 Watu wakimwamini Mungu, na kupitia maneno ya Mungu, kwa moyo unaomheshimu Mungu, basi ndani ya watu hao kunaweza kuonekana wokovu wa Mungu, na upendo wa Mungu. Watu hawa wana uwezo wa kumshuhudia Mungu, wanaishi kwa kudhihirisha ukweli, na kile wanachokikiri ni kweli, kile Mungu Alicho, na tabia ya Mungu, na wanaishi Kati ya upendo wa Mungu na wameona upendo wa Mungu. Watu wakitaka kumpenda Mungu, lazima wauonje upendo wa Mungu, na kuuona upendo wa Mungu; hapo tu ndipo wanaweza kupata kuamshiwa moyo ndani yao ambao unampenda Mungu, moyo ambao uko tayari kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa heshima.

2 Mungu hawafanyi watu kumpenda kupitia maneno na sura, au kwa mawazo yao, na Hawalazimishi watu kumpenda. Badala yake, Anawafanya wampende kwa hiari yao, na huwafanya kuyaona mapenzi Yake katika kazi Yake na matamshi, ambapo baadaye wanakuwa na upendo wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio watu wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Watu hawampendi Mungu kwa sababu wameombwa na wengine kufanya vile, wala si msukumo wa hisia wa muda mfupi. Wanampenda Mungu kwa sababu wameuona upendo wake, na wameona kuwa kuna mengi kumhusu ambayo yanastahili upendo wao, kwa sababu wameona wokovu wa Mungu, busara, na matendo ya ajabu—na kutokana na hayo, wanamsifu Mungu kwa kweli, na kumtamani kwa kweli, na wanaamshiwa msisimko ndani yao kwamba hawawezi kuishi bila kumpata Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 763 Upendo wa Mungu Lazima Uonjwe Katika Maisha Halisi

Inayofuata: 765 Pitia Kazi ya Mungu ili Kugundua Uzuri Wake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp