696 Lazima Ujue Jinsi ya Kupitia Kazi ya Mungu

1 Kama hupitii kazi ya Mungu, basi kamwe hutaweza kufanywa mkamilifu. Ni wakati tu unaweza kupitia kazi ya Mungu na uweze kuipitia na kuitafakari wakati wowote na mahali popote, wakati unaweza kuwaacha wachungaji na uishi peke yako ukimtegemea Mungu, na uweze kuona matendo halisi ya Mungu—ni hapo tu ndipo mapenzi ya Mungu yatatimizwa. Sasa hivi, watu wengi hawajui jinsi ya kupitia, na wanapokumbana na suala, hawajui jinsi ya kulishughulikia; hawawezi kuipitia kazi ya Mungu, na hawezi kuishi maisha ya kiroho. Lazima uchukue maneno ya Mungu na kuyafanya ndani ya maisha yako ya utendaji.

2 Wakati mwingine Mungu hukupa aina fulani ya hisia, hisia inayokusababisha upoteze starehe yako ya ndani kabisa, na unapoteza uwepo wa Mungu, kiasi kwamba unatumbukia gizani. Hii ni aina ya usafishaji. Wakati wowote unapofanya kitu chochote, hicho huenda mrama, au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu. Wakati mwingine, unapofanya kitu ambacho si cha utiifu na cha uasi kwa Mungu, huenda hakuna mtu mwingine anajua kukihusu—lakini Mungu anajua. Yeye hatakuachilia, na Atakufundisha nidhamu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni yenye kina sana. Kwa makini sana Anatazama kila neno na tendo la watu, kila tendo na mwendo wao, na kila wazo lao na fikira ili watu waweze kupata ufahamu wa ndani wa vitu hivi.

3 Unafanya kitu mara moja na kinaenda mrama, unakifanya kitu tena na bado kinaenda mrama, na hatua kwa hatua utapata kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kufundishwa nidhamu mara nyingi, utajua cha kufanya ili kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu na kile kisichoambatana na mapenzi Yake. Mwishowe, utakuwa na majibu sahihi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani yako. Wakati mwingine utakuwa muasi na utakemewa na Mungu kutoka ndani. Haya yote hutoka kwa nidhamu ya Mungu. Kama huthamini neno la Mungu, kama unaidharau kazi Yake, Hatashughulika na wewe hata kidogo. Kadiri unavyoyachukulia maneno ya Mungu kwa makini, ndivyo Atakavyokupa nuru zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 695 Mtazamo wa Petro kwa Majaribio

Inayofuata: 697 Faida za Kumwamini Mungu wa Vitendo ni Kubwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp