786 Mwanadamu Amjua Mungu Kupitia Uzoefu wa Neno Lake

1 Miliki na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyatekeleza mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chemichemi na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu matokeo yaliotarajiwa ya maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia ya Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii mamlaka ya Mungu na mipango. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na katika wakati huu atakuwa pia amepata viwango tofauti vya ufahamu kumhusu Yeye.

2 Na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, uzoefu, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa dhati na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa dhati na kujua miliki na uwepo wa Mungu, anakuja na kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhakika wa kweli kuhusu, na ufafanuzi sahihi wa, ukweli wa mamlaka ya Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mkondo kamili kwa na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake. Kujali kwa mwanadamu na utii kwa Mungu kutakua kwa kiasi kikubwa, na uchaji wake Mungu utakuwa wa kweli zaidi na pia mkubwa zaidi.

3 Katika ya aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kupewa ukweli pekee na ubatizo wa uzima, bali wakati uo huo pia atapata maarifa ya kweli ya Mungu. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kubadilishwa kwa tabia yake na kupata wokovu pekee, bali pia kwa wakati huo atafikia uchaji na ibada ya kweli ya kiumbe aliyeumbwa kwa Mungu. Katika aina hii ya ushirika pekee ndio maisha ya mwanadamu yatakua kuelekea ukomavu siku baada ya siku, na ni wakati huu ndio tabia yake itabadilika polepole, na imani yake kwa Mungu, hatua kwa hatua, itatoka kwenye imani ya wasiwasi na kutoeleweka na imani isiyo ya hakika mpaka katika utii wa kweli na kujali, na kuwa katika uchaji Mungu wa kweli, na mwanadamu pia, katika mchakato wa kumfuata Mungu, ataendelea polepole kutoka kuwa mtazamaji na kuwa na hali ya utendaji, kutoka yule anayeshughulikwa na kuwa anayechukua nafasi ya kutenda; kwa aina hii ya ushirika pekee ndipo mwanadamu atafikia kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu, kwa ufahamu wa kweli wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 785 Kumjua Mungu, Lazima Ujue Maneno Yake

Inayofuata: 787 Kweli Unamwelewa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp