848 Maonyesho Yanayomilikiwa na Wale Waliokamilishwa

Watu waingiapo katika njia ya ukamilifu, tabia zao za zamani zaweza kubadilishwa. Aidha, maisha yao huendelea kukua na taratibu hujitosa zaidi katika ukweli. Wanaweza kuchukia dunia na kuwachukia wale wote ambao hawafuati ukweli. Hususan hujichukia wao wenyewe, na hata zaidi ya hayo, wanajitambua vyema. Wana hiari kuishi kulingana na ukweli na hulenga kufuata ukweli. Hawako radhi kuishi katika mawazo ya bongo zao, na huchukia kujitukuza, kujisifu, na kujiinua kwa mwanadamu. Wananena kwa adabu ya hali ya juu, wanafanya mambo kwa utambuzi na hekima, ni waaminifu na watiifu kwa Mungu. Wakipitia kuadibu na hukumu, wao hawakuwi wanyonge au wasioonyesha hisia tu, bali hutoa shukrani kwa ajili ya kuadibu na hukumu zitokazo kwa Mungu. Wanaamini hawawezi kuishi bila kuadibu na hukumu ya Mungu; wanaweza kupata ulinzi Wake kupitia haya. Hawafuati imani ya amani na furaha na ya kutafuta mkate wa kuwashibisha. Wala hawafuati raha za muda za kimwili. Hili ndilo wakamilifu huwa nalo.

Umetoholewa kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 847 Kutafuta Ukweli Ndiyo Fursa ya Pekee ya Kukamilishwa

Inayofuata: 849 Ahadi za Mungu kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp