687 Kushindwa ni Fursa Bora ya Kujijua
1 Katika imani yako, lazima ujifunze kupitia kazi ya Mungu na kumtii Mungu. Kumtii Mungu ni ukweli fulani, na ni matakwa ya Mungu kwa wanadamu. Ikiwa unaweza kutafuta katika mwelekeo wa kumtii Mungu, basi umeanza kutembea kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Kutofaulu na kuanguka mara nyingi si jambo baya; na kufunuliwa pia si jambo baya. Iwe umeshughulikiwa, kupogolewa, au kufunuliwa, lazima ukumbuke hili wakati wote: Kufunuliwa hakumaanishi kuwa unashutumiwa. Kufunuliwa ni jambo zuri; ni fursa bora zaidi kwako kupata kujijua. Kunaweza kuuletea uzoefu wako wa maisha mabadiliko ya mwendo. Bila hilo, hutamiliki fursa, hali, wala muktadha wa kuweza kufikia ufahamu wa ukweli wa upotovu wako.
2 Kama unaweza kujua vitu vilivyo ndani yako, vipengele hivyo vyote vilivyofichika ndani yako ambavyo ni vigumu kutambua na ni vigumu kufukua, basi hili ni jambo zuri. Kuweza kujijua mwenyewe kweli ndiyo fursa bora zaidi kwako kurekebisha njia zako na kuwa mtu mpya. Mara tu unapojijua mwenyewe kweli, utaweza kuona kwamba ukweli unapokuwa maisha ya mtu, ni jambo la thamani kweli, na utakuwa na kiu ya ukweli na kuingia katika uhalisi. Hili ni jambo zuri sana! Kama unaweza kunyakua fursa hii na ujitafakari mwenyewe kwa bidii na kupata ufahamu wa kweli kujihusu kila unaposhindwa au kuanguka, basi katikati ya uhasi na udhaifu, utaweza kusimama tena. Mara tu unapovuka kilele hiki, basi utaweza kuchukua hatua kubwa mbele na kuingia katika uhalisi wa ukweli.
Umetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo