192 Nimekusudia Kumridhisha Mungu kwa Uaminifu

1

Naiona siku ambayo Mungu atapata utukufu ikikaribia. Nikikumbuka yaliyopita, moyo wangu huhisi majuto sana.

Nilikuwa mwasi sana katika ushirika wangu na Mungu, kiasi kwamba nimeachwa na kumbukumbu nzito.

Najichukia kwa kupata fahamu nikiwa nimechelewa sana, nahisi hatia kwa kushindwa kulipiza upendo wa Mungu.

Hakuna nilichofanya kilichoupendeza moyo wa Mungu; ningewezaje basi kuwa na amani na furaha moyoni mwangu?

Mungu alipata mwili kufanya kazi ulimwenguni, kuishi pamoja na mwanadamu na kushiriki mateso yao.

Ni muhimu sana kwa mwanadamu kumpenda Mungu, najichukia kwa kukosa dhamiri au mantiki.

Ninahisi kuwa mdeni mkubwa kwa Mungu kwa kushindwa kumpenda kwa dhati.

2

Nafurahia sana upendo wa Mungu, moyo wangu unatamani kumlipiza Mungu hivi karibuni.

Lakini asili yangu inaasi na sitendi ukweli, nimepoteza nafasi nyingi za kukamilishwa.

Sijaachwa na chochote ila toba na majuto, najichukia na kujikirihi hata zaidi.

Naona kuwa sina uhalisi wa ukweli, na bado niko hobelahobela sana katika kutenda wajibu wangu.

Moyo wangu unahangaika, nalia machozi machungu, nahisi moyoni kuwa siwezi kumkabili Mungu.

Kupitia kuhesabu neema ya Mungu kwa uangalifu, naona jinsi Mungu alivyo mzuri na wa kupendeza.

Mungu analipa gharama ya juu sana kuniokoa, hivyo kwa nini siwezi kulipiza upendo Wake?

Ingawa sijatupa kabisa upotovu, nitafanya niwezalo kufuatilia ukweli.

Katika mkondo wa mwisho wa njia, natamani kumridhisha Mungu kwa uaminifu.

Iliyotangulia: 191 Jinsi ya Kurudisha Wokovu Uliopotea

Inayofuata: 193 Wimbo wa Onyo Jema

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki