741 Mche Mungu Upate Ulinzi Wake

1 Kuwa wa utendaji katika tabia na matendo yako, kutoachana na sala katika jambo lolote unalofanya, kuja mara kwa mara mbele za Mungu, na kamwe kutopotea kutoka kwa Mungu—hii ni misingi ya kumwamini Mungu! Haijalishi maisha yako yalivyo makuu, kimo chako kilivyo kikuu, au ni kiasi kipi cha uhalisi wa ukweli ambao umeingia, moyoni mwako lazima usimwache Mungu; lazima usipotee kutoka kwa Mungu. Unaweza kusema, “Sitapotea mbali sana na Mungu; Nitaondoka kwa muda mfupi tu, sawa?” Haya ni maneno gani? Hili sio suala la karibu au mbali; ukiwa bila Mungu moyoni mwako wakati wowote, basi tayari umepotea mbali na Mungu. Watu wapoteao kutoka kwa Mungu mara nyingi hawamchi.

2 Watu wanapopotea mbali na Mungu, athari ni gani? Mara wanapofanya hivyo, wanakuwa na uwezekano wa kuwa watumwa wa Shetani wakati wowote. Baada ya hapo, watafichua tabia yao ya kishetani kupitia katika maneno na matendo yao. Mara nyingi watafanya makosa, na kumwasi Mungu mara kwa mara, na watatatiza na kuvuruga maisha ya kanisa. Wakati wowote, wako katika hatari ya kutumiwa na kutekwa nyara na Shetani—jambo la kutisha lililoje! Hivyo, ni usipopotea kutoka kwa Mungu moyoni mwako tu na uweze kuishi mbele za Mungu wakati wote ndipo unaweza kuwa mtu anayemcha Mungu, na mara tu unapokuwa na akili hii ndipo Mungu anaweza kukulinda dhidi ya kuchukua njia mbaya.

Umetoholewa kutoka katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 740 Ni Wale tu Wanaomcha Mungu Ndio Wanaweza Kumshuhudia Katika Majaribio

Inayofuata: 742 Ni Wale tu Wanaomcha Mungu Ndio Wenye Furaha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp