995 Sifa za Mabadiliko ya Tabia

1 Mabadiliko katika tabia yana sifa chache bainifu. Moja ni kuweza kukubali ukweli na kutii kile ambacho ni sahihi na kinacholingana na ukweli. Haijalishi ni nani anayekupa mapendekezo—wawe ni vijana au wazee, iwe mnashirikiana vizuri, na iwe kuna visasi kati yenu—alimradi anasema kitu kilicho sahihi na kinacholingana na ukweli, na chenye manufaa kwa kazi ya familia ya Mungu, basi unaweza kukichukua na kukikubali, na usiathiriwe na mambo mengine yoyote. Hii ndiyo sifa ya kwanza bainifu. Sifa nyingine bainifu ni kuweza kutafuta ukweli wakati wowote unapokumbana na shida. Kwa mfano, ukikumbana na shida mpya ambayo hakuna mtu anaweza kuielewa, unaweza kutafuta ukweli, uone ni nini unachopaswa kutenda ili kufanya jambo hilo lilingane na kanuni za ukweli, na kinatosheleza mahitaji ya Mungu.

2 Sifa nyingine bainifu ni kupata uwezo wa kufikiria mapenzi ya Mungu. Bila kujali ni mahitaji yapi ambayo Mungu anayo kwako katika wajibu wako, unaweza kuutekeleza kulingana na kile ambacho Mungu anahitaji, kutenda kwa jitihada ya kumridhisha Mungu, na kutenda kwa kuwajibika na uaminifu.Yote haya ni njia ya kufikiria mapenzi ya Mungu. Kama hujui jinsi ya kufikiria mapenzi ya Mungu katika jambo unalotenda, lazima ufanye utafutaji fulani ili kukamilisha hilo, na kumridhisha Yeye. Ikiwa mnaweza kuweka kanuni hizi tatu katika vitendo, mpime njia ambayo kwa kweli mnaishi kulingana nazo, na kupata njia ya kutenda, basi mtakuwa mnayashughulikia mambo kwa njia yenye maadili. Bila kujali unalokabiliana nalo na bila kujali ni shida gani unazolazimika kushughulikia, ikiwa unaweza kuzipata kanuni za kutenda, basi utaweza kutenda ukweli kwa urahisi.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kuweka Ukweli Katika Vitendo Tu Ndipo Unaweza Kutupa Minyororo ya Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 994 Mungu Hatimaye Huwapata wale Walio na Ukweli

Inayofuata: 996 Unapaswa Kutafuta Kuwa Nusura

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki