491 Pigana Mapigano Mazuri kwa Ajili ya Ukweli

1 Kama unataka kupigana vita vizuri kwa ajili ya ukweli, basi kwanza kabisa, usimpe Shetani nafasi ya kufanya kazi, na ili kufanya hivi mtastahili kuwa na nia moja na muweze kutumika katika kushirikiana, acheni dhana zenu za kibinafsi, maoni, mitazamo na njia za kufanya mambo, tuliza moyo wako ndani Yangu, zingatia sauti ya Roho Mtakatifu, kuwa makini na kazi ya Roho Mtakatifu na uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu kwa kina. Lazima uwe na nia moja tu, ambayo ni kwamba mapenzi Yangu yaweze kutendeka. Hupaswi kuwa na nia nyingine. Lazima uangalie Kwangu kwa moyo wako wote, angalia hatua Zangu na Ninavyotenda mambo kwa karibu, na wala usiwe mzembe kabisa.

2 Roho yako lazima iwe amilifu, macho yako yakiwa wazi. Kwa kawaida, wale ambao nia na malengo yao si sahihi, wale ambao wanapenda kuonekana na wengine, wenye hamu ya kutenda mambo, wenye tabia ya kukatiza, walio imara katika mafundisho ya dini, watumishi wa Shetani, nk., watu hawa wanapoinuka wanakuwa ugumu kwa kanisa na kula na kunywa kwa ndugu kunakuwa si kitu; unapompata mtu wa aina hii jifanye kisha mpige marufuku mara moja. Kama muda baada ya muda hawabadiliki basi watateseka sana. Kama wale wanaoendelea katika njia zao kwa ukaidi wanajitetea na kujaribu kufunika dhambi zao, kanisa linapaswa kuwaondoa mara moja na kutowaachia nafasi ya kuendelea. Usipoteze mengi kwa kujaribu kuokoa machache, na uzingatie makubwa.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 17” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 489 Yachukulie Maneno ya Mungu kama Msingi wa Matendo Yako

Inayofuata: 493 Zingatia Maneno ya Mungu kwa Ajili ya Uhusiano Ufaao na Wengine

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki