480 Yajaze Maisha Yako na Neno la Mungu

1 Kuanzia sasa kuendela, mazungumzo ya maneno ya Mungu yanapaswa kuwa kanuni ambayo kwayo unazungumza. Kwa kawaida, mnapojumuika pamoja, mnapaswa kushiriki katika ushirika kuhusu maneno ya Mungu, mkiyachukua maneno ya Mungu kama maudhui ya mwingiliano wenu, mkiongea juu ya yale mnayojua kuhusu maneno haya, jinsi mnavyoyaweka katika vitendo, na jinsi Roho Mtakatifu afanyavyo kazi. Alimradi unashiriki maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Kufanikisha ulimwengu wa maneno ya Mungu kunahitaji ushirikiano wa mwanadamu. Usipoingia katika hili, Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi; ukiufunga mdomo wako na usizungumze kuhusu maneno Yake, Hatakuwa na njia ya kukuangazia.

2 Wakati wowote ambapo huna shughuli nyingine, zungumza juu ya maneno ya Mungu, na usijishughulishe na mazungumzo yasiyo na maana! Acha maisha yako yajazwe na maneno ya Mungu—ni hapo tu ndipo utakapokuwa mwumini mwenye kumcha Mungu. Haijalishi ikiwa ushirika wako ni wa juu juu. Bila ujuu juu hakuwezi kuwepo kina kirefu. Lazima kuwe na mchakato. Kupitia mafunzo yako, utafahamu kuangaziwa kwako na Roho Mtakatifu, na jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu kwa matokeo yanayotarajiwa. Baada ya muda wa uchunguzi, utaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ni ukiamua kushirikiana tu ndipo utaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 479 Mtazamo Anaopaswa Kuwa Nao Mtu kwa Maneno ya Mungu

Inayofuata: 481 Jinsi Mwanadamu Anavyopaswa Kutembea Katika Njia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp