508 Lenga Kutenda Ukweli Ili Ukamilishwe

1 Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua nakutia ukweli katika vitendo. Mungu hakika atakubariki, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu.

2 Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu hufanikishwa daima anapojua hali yake mwenyewe halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko tayari kujijua na yuko tayari kuwasiliana ataweza kutekeleza ukweli. Aina hii ya mtu ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe ni wa kina au wa juu juu, haba au maridhawa. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe.

3 Mtu ambaye ana maarifa ya Mungu ni yule ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana hakika kuhusu mwili wa Mungu, na ana hakika kuhusu neno la Mungu na kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi au kuzungumza, au jinsi watu wengine husababisha vurugu, anaweza kushikilia msimamo wake, na kuwa shahidi kwa Mungu. Kadiri mtu alivyo katika njia hii ndivyo anavyoweza kutekeleza zaidi ukweli anaouelewa. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, yeye hupata ufahamu zaidi wa Mungu, na analo azimio la kuwa shahidi kwa Mungu milele.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 507 Ni kwa Kuishi kwa Kudhihirisha Uhalisi tu Ndiyo Unaweza Kutoa Ushahidi

Inayofuata: 509 Watu Wanaopatwa na Mungu Wamemiliki Uhalisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp