523 Fuata Maneno ya Mungu na Huwezi Kupotea

1 Mungu anatumaini mnaweza kula na kunywa peke yenu, na kila wakati muishi katika nuru ya uwepo wa Mungu, na kwa njia mnayoishi, kamwe msiyaache maneno ya Mungu; hapo tu ndipo mtakapoweza kujazwa na maneno ya Mungu. Katika kila neno na tendo lako, maneno ya Mungu hakika yatakuongoza mbele. Ukimkaribia Mungu kwa dhati kwa kiwango hiki, utaweza kuwasiliana na Mungu kila wakati, na hakuna chochote ufanyacho kitakachoishia katika mkanganyiko au kukuacha ukihisi usiyejua chochote. Bila shaka utaweza kuwa na Mungu upande wako, utaweza daima kutenda kulingana na neno la Mungu.

2 Na kila mtu, jambo, na kitu unachokutana nacho, neno la Mungu litakuonekania wakati wowote, likikuongoza utende kulingana na mapenzi Yake. Fanya kila kitu katika neno la Mungu, na Mungu atakuongoza mbele katika kila kitendo chako; hutapotea kamwe, na utaweza kuishi katika nuru mpya, na nuru mpya na nyingi zaidi. Huwezi kutumia mawazo ya kibinadamu kufikira kuhusu cha kufanya; unapaswa kutii mwongozo wa neno la Mungu, uwe na moyo safi, uwe kimya mbele za Mungu, na utafakari zaidi. Usifadhaike kuhusu suluhisho kwa kile usichoelewa; yalete mambo kama hayo mbele za Mungu mara nyingi, na umtoelee moyo wa dhati.

3 Amini kuwa Mungu ndiye mwenyezi wako! Lazima uwe na azimio kubwa kwa Mungu, ukitafuta kwa nguvu huku ukikataa visingizio, nia, na hila za Shetani. Usikate tamaa. Usiwe dhaifu. Tafuta kwa moyo wako wote; subiri kwa moyo wako wote. Shirikiana kwa vitendo na Mungu, na ujiondolee vikwazo vyako vya ndani.

Umetoholewa kutoka kwa ushirika wa Mungu

Iliyotangulia: 522 Ishi Katika Maneno ya Mungu ili Uwe na Kazi ya Roho Mtakatifu

Inayofuata: 524 Neno la Mungu Kweli Limekuwa Maisha Yako?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp