996 Jinsi ya Kufuata Vizuri Hatua ya Mwisho ya Njia

1 Lazima ukumbuke kwamba maneno haya sasa yamenenwa: Baadaye, utapitia dhiki kubwa na mateso makubwa! Kukamilishwa silo jambo rahisi au jepesi. Angalau lazima uwe na imani ya Ayubu, au hata labda imani kubwa kuliko yake. Unapaswa kujua kwamba majaribu katika siku zijazo yatakuwa makubwa kuliko majaribu ya Ayubu, na kwamba lazima bado upitie kuadibu kwa muda mrefu. Je, hili ni jambo rahisi? Ikiwa ubora wa tabia yako hauwezi kuboreshwa, ikiwa uwezo wako wa kuelewa umepungukiwa, na ikiwa unajua kidogo sana, basi wakati huo hutakuwa na ushuhuda wowote, lakini badala yake utakuwa kichekesho, kitu cha Shetani kuchezea. Ikiwa huwezi kushikilia maono sasa, basi huna msingi hata kidogo na katika siku zijazo utatupwa!

2 Hakuna sehemu ya njia ambayo ni rahisi kutembea, kwa hivyo usiichukulie kwa urahisi. Lipime hili kwa uangalifu sasa na ufanye maandalizi ili uweze kuitembea vizuri sehemu ya mwisho ya njia hii. Hii ndiyo njia ambayo lazima itembewe katika siku zijazo, njia ambayo lazima watu wote waitembee. Lazima usikose kusikiliza maarifa haya; usifikirie kuwa kile Ninachokuambia si chote cha maana. Siku itakuja ambapo utayatumia vizuri—maneno Yangu hayawezi kunenwa bure. Huu ndio wakati wa wewe kujiandaa, wakati wa kuandaa njia kwa ajili ya siku zijazo. Unapaswa kuandaa njia ambayo unapaswa kuitembea baadaye; unapaswa kuwa na hofu na wasiwasi kuhusu jinsi utakavyoweza kusimama imara katika siku zijazo na ujiandae vizuri kwa ajili ya njia yako ya baadaye. Usiwe mlafi na mvivu!

3 Lazima ufanye kila kitu uwezacho kabisa kutumia muda wako vizuri, ili uweze kupata kila kitu unachohitaji. Ninakupa kila kitu ili uweze kuelewa. Kwa kupitia dhiki kubwa zaidi, ufahamu wa kweli ndani ya watu wote utatimizwa. Hizi ni hatua za kazi. Punde unapofahamu kikamilifu maono yaliyoshirikiwa leo na ufikie kimo cha kweli, basi ugumu wowote utakaopitia katika siku zijazo hautakushinda na utaweza kuustahimili. Nitakapokuwa nimemaliza hatua hii ya mwisho ya kazi na kumaliza kunena maneno ya mwisho, katika siku zijazo watu watahitajika kutembea njia yao wenyewe. Hili litatimiza maneno yaliyonenwa hapo awali: Roho Mtakatifu ana agizo kwa kila mtu, na kazi ya kufanya ndani ya kila mtu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Sehemu ya Mwisho ya Njia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 995 Lazima Uthamini Baraka za Leo

Inayofuata: 997 Mungu Anapompiga Mchungaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp