393 Fuata Njia Iongozwayo na Roho Mtakatifu Katika Imani Yako

1 Mmetembea tu sehemu ndogo sana ya njia ya muumini katika Mungu, na bado hamjaingia kwenye njia sahihi, kwa hiyo bado mko mbali na kutimiza kiwango cha Mungu. Hivi sasa, kimo chenu hakitoshi kuyakidhi mahitaji Yake. Kwa sababu ya ubora wenu wa tabia na vilevile asili yenu ya maumbile ya upotovu, nyinyi daima huichukulia kazi ya Mungu kwa uzembe na hamuichukulii kwa uzito. Hii ni dosari yenu kubwa zaidi.

2 Zaidi ya hayo, hamwezi kuipata njia ya Roho Mtakatifu. Wengi wenu hamuifahamu na hamwezi kuiona kwa dhahiri. Zaidi ya hayo, wengi wenu hamtilii maanani suala hili, na hata hamlichukulii kwa uzito. Mkiendelea kufanya hivi na msipoijua kazi ya Roho Mtakatifu, basi njia ambayo mnaichukua kama muumini katika Mungu itakuwa bure. Hii ni kwa sababu hamfanyi kila liwezekanalo ili kutafuta kutimiza mapenzi ya Mungu, na pia kwa sababu hamshirikiani vizuri na Mungu. Sio kwamba Mungu hajawafanyia kazi, au kwamba Roho Mtakatifu hajawasisimua. Ni kuwa nyinyi ni wazembe sana kiasi kwamba hamuichukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa uzito. Lazima mbadilike mara moja na kutembea njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu.

3 “Njia hii inayoongozwa na Roho Mtakatifu” ni ili watu wapate nuru katika roho zao, wawe na ufahamu wa neno la Mungu, wapate ufahamu kuhusu njia iliyo mbele yao, na waweze kuingia katika ukweli hatua kwa hatua, na kuja kumwelewa Mungu zaidi na zaidi. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu hasa ni kwamba watu wawe na ufahamu zaidi wa neno la Mungu, bila mikengeuko na kuelewa kubaya, ili waweze kutembea ndani yake. Ili kutimiza athari hii, mtahitaji kufanya kazi kwa upatanifu na Mungu, kutafuta njia sahihi ya kutia katika vitendo, na kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii inahusu ushirikiano kwa upande wa mwanadamu, yaani, mnachofanya kutimiza mahitaji ya Mungu kwenu, na jinsi mnavyotenda ili kuingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Maisha ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 392 Watu Wanapaswa Kumwamini Mungu kwa Moyo Unaomwogopa Mungu

Inayofuata: 394 Lazima Uweke Imani Katika Mungu Juu ya Vingine Vyote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp