217 Ifuate Kazi Mpya ya Roho Mtakatifu na Kupata Sifa ya Mungu

1 “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu.

2 Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli.

3 Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 216 Wamebarikiwa Wale Wanaokubali Kazi Mpya ya Mungu

Inayofuata: 218 Itii Kazi ya Roho ili Kufuata Hadi Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp