190 Hukumu Iliuzindua Moyo Wangu

1

Nitafute nini katika imani yangu?

Sasa nimepata mzinduko.

Hapo awali nilimwamini Bwana ili kubarikiwa tu.

Kwa pupa nilifurahia neema ya Mungu.

Lakini hukumu iliuzindua moyo wangu.

2

Nilisema mambo yote yanayofaa katika maombi

lakini nilitenda chochote nilichotaka.

Nilichomfanyia Bwana ilikuwa kwa ajili ya siku zangu za usoni na majaliwa tu.

Sikutenda ukweli kabisa.

Kisha hukumu iliuzindua moyo wangu

Nilimwabudu Mungu nikiishi katika ibada za dini tu

lakini nilikuwa mtupu moyoni, sikujazwa.

Tabia yangu potovu haikutakaswa.

Ningewezaje kutekeleza mapenzi ya Mungu?

Maneno ya Mungu ni kama upanga ukatao kuwili,

unaouchoma moyo na roho yangu.

Nimeteseka sana kupitia majaribio na kusafishwa,

tabia yangu potovu imetakaswa.

Nimeonja upendo wa Mungu na ninakusudia

kutafuta na kupata ukweli.

Nitatimiza wajibu wangu kwa uaminifu,

kulipiza upendo Wake na kuwa shahidi Wake wa kweli.

3

Katika imani yangu nimefurahia neema ya Mungu,

lakini haimaanishi nimepata uzima.

Bila ukweli siwezi kuishi kwa kudhihirisha uhalisi,

kusema nilimpenda Mungu ulikuwa uongo.

Lakini hukumu iliuzindua moyo wangu.

4

Bila kujali ninavyoabudu au matendo mengi mema niliyo nayo.

Nilikuwa mnafiki.

Kazini niliafikiana na Mungu,

nikimdanganya na kumpinga Yeye kwa kweli.

Kisha hukumu iliuamsha moyo wangu.

Nimeona jinsi nilivyopotoshwa sana.

Na nahitaji hukumu na utakaso Wake.

Nimehukumiwa mbele ya kiti cha Kristo,

Na moyo wangu umezinduliwa.

Maneno ya Mungu ni kama upanga ukatao kuwili,

unaouchoma moyo na roho yangu.

Nimeteseka sana kupitia majaribio na kusafishwa,

tabia yangu potovu imetakaswa.

Nimeonja upendo wa Mungu na ninakusudia

kutafuta na kupata ukweli.

Nitatimiza wajibu wangu kwa uaminifu,

kulipiza upendo Wake na kuwa shahidi Wake wa kweli.

Iliyotangulia: 189 Kugutuka Kupitia Hukumu

Inayofuata: 191 Maneno ya Mungu Yaliuzindua Moyo Wangu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp