503 Unyime Mwili ili Kuona Uzuri wa Mungu

1 Ikiwa unampenda Mungu kwa dhati, na huuridhishi mwili, basi utaona kuwa kila anachokifanya Mungu ni chenye haki sana, na kizuri sana, na kwamba laana Yake kwa uasi wako na hukumu ya udhalimu wako ni haki. Zitakuwepo nyakati ambapo Mungu atakurudi na kukufundisha nidhamu, na kuanzisha mazingira ya kukukasirisha, na kukushurutisha uje mbele Zake—na daima utahisi kuwa anachokifanya Mungu ni cha ajabu. Hivyo utahisi kana kwamba hakuna uchungu mwingi, na kwamba Mungu anapendeza.

2 Ukifuata udhaifu wa mwili, na kusema kwamba Mungu amezidi, basi daima utahisi uchungu na daima utahuzunika, na utakosa uwazi kuhusu kazi yote ya Mungu na itaonekana kana kwamba Mungu hana huruma kwa udhaifu wa mwanadamu, na Hatambui shida za mwanadamu. Hivyo utajihisi mnyonge na mpweke, kana kwamba umekumbwa na dhuluma kubwa, na wakati huo utaanza kulalama.

3 Kadiri unavyoutosheleza udhaifu wa mwili, ndivyo unavyohisi kuwa Mungu anazidi, hadi inakuwa mbaya kiasi kwamba unaikana kazi ya Mungu, na kuanza kumpinga Mungu na kujaa uasi. Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: “Mume wangu(mke), watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani! Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Lazima uwe na azimio hili.

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 502 Maana ya Kuunyima Mwili

Inayofuata: 504 Kuteseka kwa Ajili ya Kutenda Ukweli ni kwa Maana Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp