Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Kanuni Nne

1 Mwanadamu “ananipenda”, si kwa sababu upendo wake Kwangu Mimi ni wa asili, lakini kwa sababu anaogopa kuadibu. Nani kati ya wanadamu alizaliwa akinipenda? Ni nani ananitendea kama kwamba Mimi ni moyo wake mwenyewe? Na kwa hiyo Najumlisha hili na neno la hekima kwa ulimwengu wa binadamu: Miongoni mwa wanadamu, hakuna yeyote anayenipenda. Naweza kumpenda mwanadamu milele, na pia Naweza kumchukia milele, na hili kamwe halitabadilika, kwani Nina ustahamilivu. Lakini mwanadamu hana ustahamilivu huu, yeye kila mara hughairighairi Kwangu. Hivyo, Mimi hufupisha hili katika methali nyingine: Watu hukosa ustahimilivu, na hivyo hawawezi kuutimiza moyo Wangu.

2 Leo, bado Sijui ni kwa nini mwanadamu hazingatii wajibu wake, kwa nini hajui jinsi kimo chake kilivyo kikubwa. Watu hata hawajui kama ni gramu kadhaa au liang kadhaa. Na hivyo, bado wao wananidanganya. Ni kana kwamba kazi Yangu yote imekuwa bure, kana kwamba maneno Yangu ni mwangwi ndani ya milima mikubwa, na hakuna ambaye amewahi kutambua asili ya maneno na matamko Yangu. Na kwa hiyo Natumia hili kama msingi wa kufanya muhtasari wa methali ya tatu: Watu hawanijui, kwa kuwa hawanioni.

3 Watu hulia kwa sababu ya maneno Yangu, na maombi yao kila mara huwa na manung’uniko kuhusu ukatili Wangu. Ni kana kwamba wote wanatafuta “upendo” Wangu wa kweli kwa mwanadamu—lakini wangewezaje kupata upendo Wangu katika maneno Yangu makali? Kutokana na hilo, wao kila mara hukata tamaa kwa sababu ya maneno Yangu. Mbona, katika kile wasemacho, watu daima hulalamika kunihusu? Hivyo, Nafanya muhtasari wa methali ya nne ya maisha ya mwanadamu: Watu hunitii kiasi kidogo tu, na hivyo wao kila mara hunichukia.

4 Ninapowahitaji kufanya mambo fulani, wao hushangaa: Hawakuwa wamewahi kufikiri kwamba Mungu, ambaye Amekuwa mwenye ukarimu na mwenye huruma kwa miaka mingi sana, Angeweza kusema maneno kama hayo, maneno ambayo ni ya kikatili na yasiyothibitika, na kwa hiyo wao huduwaa. Nyakati kama hizo, Naona kwamba chuki iliyo ndani ya mioyo ya watu Kwangu imekua mara nyingine, kwa sababu wameanza tena kazi ya kulalamika. Wao kila mara huilaumu dunia na kulaani Mbinguni. Lakini katika maneno yao, Sioni chochote kinachowalaani wao wenyewe kwa sababu wanajipenda sana. Hivyo Nafanya muhtasari wa maana ya maisha ya mwanadamu: Kwa kuwa watu wanajipenda kupita kiasi, maisha yao yote ni ya uchungu na matupu, na wao huwa na uharibifu wa kujitakia kotekote kwa sababu ya chuki yao Kwangu.

Umetoholewa kutoka katika Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Wasiofuatilia Ukweli Hawawezi Kufuata Hadi Mwisho

Inayofuata:Watu Hawajui Wokovu wa Mungu

Maudhui Yanayohusiana

 • Upendo Safi Bila Dosari

  I Upendo ni hisia safi, safi bila dosari. Tumia moyo, tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga. Tumia moyo, …

 • Upendo wa Kweli wa Mungu

  I Nasimama mbele ya Mungu wangu tena leo. Moyo wangu una mengi ya kusema ninapoona uso Wake wa kupendeza. Nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura ny…

 • Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu

  Ⅰ Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda, uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme. Maneno Yako yamenitakasa mimi,…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…