605 Kupatwa na Mungu Kunategemea Ufuatiliaji Wako Mwenyewe

1 Yote ambayo Petro alitafuta yalikuwa kufuata Moyo wa Mungu. Alitaka kutimiza mapenzi ya Mungu, na licha ya taabu na mashaka, bado yeye alikuwa tayari kutimiza mapenzi ya Mungu. Hakuna ukimbizaji mkuu zaidi wa muumini katika Mungu. Kile ambacho Paulo alitafuta kilitiwa doa na mwili wake, na dhana zake mwenyewe, na mipango na mipangilio yake mwenyewe. Hakuwa kwa njia yeyote kiumbe wa Mungu aliyehitimu, hakuwa mtu ambaye alitaka kutimiza mapenzi ya Mungu. Petro alitaka kujiwasilisha kwenye mipango ya Mungu, na ingawa kazi aliyofanya haikuwa kuu, motisha ya harakati yake na njia ambayo alitembea zilikuwa sahihi; ingawa hakuweza kupata watu wengi, aliweza kufuata njia ya ukweli. Kwa hivyo inaweza kusemwa kwamba alikuwa kiumbe wa Mungu aliyehitimu.

2 Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. Iwapo ulifanya kazi nyingi, na watu wengine walipata mafundisho yako, lakini wewe mwenyewe hukubadilika, na hukuwa na ushuhuda wowote, au kuwa na uzoefu wowote wa kweli, kwa namna kuwa katika hatima ya maisha yako, bado hakuna yoyote uliyofanya iliyo na ushuhuda, basi je, wewe ni mtu aliyebadilika? Je, wewe ni mtu ambaye hufuatilia ukweli?

3 Wale walio najisi hawakubaliki kuingia katika ufalme, wale walio najisi hawakubaliki kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na umefanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mwovu kupindukia—hakuvumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba wewe unataka kuingia katika ufalme wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijatoa njia rahisi ya kuingilia ufalme Wangu kwa wale wenye neema Yangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja. Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu.

Umetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 604 Kile Ambacho Anayemwamini Mungu Anapaswa Kufuatilia

Inayofuata: 606 Mungu Hutumia Asili ya Mwanadamu Kumpima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp