55 Amkeni na Kumchezea Mungu

1

Tumesikia sauti ya Mungu na kuinuliwa mbele Yake ili kuhudhuria karamu.

Tunakula na kunywa maneno ya Mungu na kuomba Kwake, kuishi mbele Yake ni furaha kubwa.

Tulipomwamini Bwana ndani ya dini, mioyo yetu ilikuwa ya giza na hatukuwa na njia.

Sasa tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunashiriki kuhusu ukweli. Kufurahia kazi ya Roho Mtakatifu ni furaha sana.

Ndugu na dada, simameni na mcheze! Toeni densi mpya kumsifu Mungu!

Tumetoroka minyororo ya kaida za dini, tumeelewa ukweli na roho zetu zimefunguliwa.

Maneno yote ya Mungu ni ukweli, yanatuonyesha njia katika maisha.

Hatutawahi tena kufanya hila kwa ajili yetu, tutatii utawala wa Mungu na mipangilio kabisa.

2

Tumepitia hukumu ya maneno ya Mungu, upotovu wetu umetakaswa na kubadilishwa.

Tunaishi kama watoto wasio na hatia, na tunamwabudu Mungu kwa roho na ukweli.

Maneno ya Mungu yakituongoza, tunakanyaga ukandamizaji wote na shida chini ya visigino vyetu.

Haijalishi anavyotuzuia Shetani, tutamfuata Kristo na kuwa waaminifu hadi mwisho.

Ndugu, amkeni na mcheze! Toeni densi mpya kumsifu Mungu!

Kumfuata Kristo ni furaha ya kweli, njia inang’aa zaidi na zaidi.

Kwa kujua haki na utakatifu wa Mungu, moyo wangu unataka tu kumsifu.

Kumtukuza Mungu ni furaha, Yeye kuwa pamoja nasi ni furaha ya kweli.

Kumshuhudia Mungu ni utukufu wa kweli, roho yangu ni huru sana.

Msifu Mungu kwa kumshinda Shetani, Amepata utukufu wote.

Iliyotangulia: 54 Mtukuze Mwenyezi Mungu Kwa Sauti Kubwa

Inayofuata: 57 Kazi Kuu ya Mungu Imekamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki