237 Achana na Dhana za Kidini ili Kufuata Nyayo za Mungu

1 Katika imani yako kwa Mungu, utamjuaje Mungu? Unapaswa kumjua Mungu kupitia maneno na kazi ya leo ya Mungu, bila upotovu au uwongo, na hata kabla jambo lolote lile ni sharti uijue kazi ya Mungu. Huu ndio msingi wa kumjua Mungu. Huo uwongo wa aina mbalimbali unaokosa ukubalifu wa maneno ya Mungu ni dhana za kidini, ni ukubalifu ambao ni potovu na wenye makosa. Ujuzi mkubwa zaidi wa watu mashuhuri wa kidini ni kuyachukua maneno ya Mungu yaliyokuwa yakikubalika zamani na kuyalinganisha na maneno ya Mungu ya leo. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini.

2 Walio na dhana za kidini hawana njia ya kuendelea sawia na hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, watakuwa nyuma hatua moja, halafu mbili—kwani hizi dhana za kidini humfanya mwanadamu kuwa mtu wa kujitukuza na mwenye kiburi. Mungu hahisi kumbukumbu kwa ajili ya Alichokinena na kukifanya hapo zamani; kama kimepitwa na wakati, basi Anakiondoa. Hakika unaweza kuziacha dhana zako? Ukiyakatalia maneno aliyoyanena Mungu hapo zamani, je hili linadhihirisha kuwa unaijua kazi ya Mungu? Kama huwezi kukubali mwangaza wa Roho Mtakatifu leo na badala yake unashikilia mwangaza wa zamani, hili laweza kuthibitisha kuwa unafuata nyayo za Mungu? Je, bado huwezi kuziacha dhana za kidini? Ikiwa ndivyo ilivyo, basi utakuwa mpinga Mungu.

3 Mwanadamu akiacha dhana za kidini, basi hatatumia akili yake kuyapima maneno na kazi ya Mungu leo hii, na badala yake atatii moja kwa moja. Japokuwa kazi ya Mungu ya leo inaonekana wazi tofauti na ya zamani, unaweza kuiacha mitazamo ya zamani na kutii moja kwa moja kazi ya Mungu leo hii. Kama unaweza kuwa na ufahamu kama huu kwamba unaionea fahari nafasi ya kazi ya Mungu leo bila kujali Alivyofanya kazi zamani, basi wewe ni mtu aliyeyaacha dhana zake, anayemtii Mungu na anayeweza kuitii kazi na maneno ya Mungu na kufuata nyayo za Mungu. Katika hili, kwa hakika, utakuwa mtu anayemtii Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 236 Wale Wasioikubali Kazi Mpya ya Roho Mtakatifu Wanaweza Kuona Kuonekana kwa Bwana?

Inayofuata: 238 Mwanadamu Atawezaje Kumwona “Bwana Yesu Mwokozi” Akishuka Kutoka Mbinguni?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp