628 Achana na Fikira za Kidini ili Ukamilishwe na Mungu

1 Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao. Kama kweli unataka kukamilishwa, basi lazima uamue kutupilia mbali kabisa kila kitu cha kale. Hata kama kile kilichokuwa kimefanywa awali kilikuwa sahihi, hata kama ilikuwa ni kazi ya Mungu, ni lazima bado uweze kuiweka pembeni na uache kuishikilia. Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyo wazi, iliyofanywa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, leo lazima uiweke pembeni. Hufai kuishikilia. Hili ndilo Mungu anahitaji. Kila kitu lazima kifanywe upya.

2 Katika kazi ya Mungu na neno la Mungu, Harejelei vitu vya kale ambavyo vilishapita, na vilevile Hafukui historia ya kale. Mungu siku zote ni mpya na kamwe si mzee. Hashikilii hata maneno Yake mwenyewe ya kitambo inayoonyesha kwamba Mungu hafuati mafundisho ya dini yoyote. Katika hali hii, kama mwanadamu, kama siku zote unashikilia kabisa vitu vya kale, ukikataa kuviachilia na kuvitumia kwa njia ya fomyula, huku naye Mungu hafanyi kazi tena katika njia Alizokuwa akifanya awali, basi maneno yako na matendo yako siyo ya kukatiza? Je, hujawa adui wa Mungu? Je, uko radhi kuyaacha maisha yako yote yaharibike kwa sababu ya mambo haya ya kale? Mambo haya ya kale yatakufanya kuwa mtu anayezuia kazi ya Mungu. Je, mtu kama huyo ndiye wewe unataka kuwa? Kama kweli hutaki kuwa hivyo, basi acha mara moja kile unachofanya na ubadilike; anza tena upya. Mungu hakumbuki huduma yako ya kale.

Umetoholewa kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 627 Kushikilia Fikira za Kidini Kutakuangamiza tu

Inayofuata: 629 Umeacha Fikira Zako za Kidini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp