433 Unapoutoa moyo wako kwa Mungu
1 Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako.
2 Unapompa Mungu moyo wako, katika upande chanya, unaweza kupata uingiaji wa kina zaidi na ufikie kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi. Kubadilisha tabia ya mtu ni mchakato wa mtu kuutoa kabisa moyo wake kwa Mungu, na wa kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa maneno ya Mungu. Unapoweza kuutoa moyo wako kwa Mungu, utaweza kuhisi kila harakati yenye hila ndani ya roho yako, nawe utajua kila nuru na mwangaza upokelewao kutoka kwa Mungu. Shikilia hili, nawe utaingia katika njia ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu hatua kwa hatua.
Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili