14 Mungu Ameonekana Mashariki mwa Dunia na Utukufu
1 Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu?
2 Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki.
3 Na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!
Umetoholewa kutoka katika “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni” katika Neno Laonekana katika Mwili