711 Matendo Mazuri si Sawa na Badiliko Katika Tabia

1 Mungu anapofanya kazi ili kumwokoa mwanadamu, si kwa ajili ya kumpamba mwanadamu kwa mwenendo mzuri—kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kubadilisha tabia za watu, kuwafanya wazaliwe na kuwa watu wapya. Hivyo, hukumu ya Mungu, kuadibu, majaribu, na usafishaji wa mwanadamu vyote ni kwa ajili ya kuibadilisha tabia yake, ili aweze kutimiza utii na uaminifu kamili kwa Mungu, na kumwabudu Mungu kwa kawaida. Hili ndilo lengo la kazi ya Mungu.

2 Kuwa na tabia nzuri si sawa na kumtii Mungu, hasa si sawa na kulingana na Kristo. Mabadiliko katika tabia yanategemea mafundisho, na kuzaliwa na juhudi—hayategemei maarifa ya kweli kumhusu Mungu, ama juu ya ukweli, hasa hayategemei uongozi wa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna nyakati ambapo baadhi ya yale watu wanayofanya yanaongozwa na Roho Mtakatifu, haya si maonyesho ya maisha, sembuse kuwa sawa na kumjua Mungu.

3 Haijalishi mienendo ya mtu ni mizuri kiasi gani, haithibitishi kwamba anamtii Mungu, ama kwamba anauweka ukweli katika matendo. Mabadiliko ya tabia ni udanganyifu wa muda, ni udhihirisho wa bidii, nayo si maonyesho ya maisha hayo. Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa wako na ukweli. Bidii ya watu inaweza tu kuwafanya wazingatie mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida halisi, na mafundisho hayawezi kushikilia nafasi ya ukweli.

Umetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 710 Tabia Yako Inaweza Kubadilika Tu kwa Kutii Kazi ya Mungu

Inayofuata: 712 Maonyesho ya Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp