Umeshuhudia kuwa Bwana Yesu tayari amekuja, lakini hatuamini hilo. Tumemwamini Bwana kwa miaka mingi na daima tumekuwa tukimfanyia kazi pasipo kuchoka, kwa hiyo Bwana atakapokuja anapaswa kutufichulia kwanza. Kwa kuwa Bwana hajatufichulia jambo hilo, hiyo inatuonyesha tu kwamba Hajarudi. Tumekosea kwa kuamini hili?

08/03/2020

Aya za Biblia za Kurejelea:

Yesu akasema kwake, Tomaso, kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini” (Yohana 20:29).

“Kwa hiyo kesheni: kwa kuwa hamjui ni saa ipi ambayo Bwana wenu atakuja. … Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu” (Mathayo 24:42-44).

“Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi, na hutajua saa ambayo nitakuja kwako” (Ufunuo 3:3).

“Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6).

“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata” (Yohana 10:27).

“Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho” (Ufunuo 2:7).

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Katika kitabu cha unabii cha nabii Isaya, hakuwahi kutajwa kwamba mtoto anayeitwa Yesu angezaliwa katika enzi ya Agano Jipya; bali kuliandikwa tu kwamba mtoto mchanga wa kiume anayeitwa Imanueli angezaliwa. Mbona hakutaja jina Yesu? Hakuna pahali popote kwa Agano la Kale panapotokea jina hili, hivyo mbona basi mnamwamini Yesu? Hakika hamkumwona Yesu kwa macho yenu kabla kuja kumwamini? Ama mlianza kuamini mlipopata ufunuo? Mungu kweli angewaonyesha neema kama hiyo? Na kuwapa baraka kubwa kama hiyo? Je, ni kwa msingi gani mlimwamini Mungu? Mbona basi hamwamini kwamba Mungu amekuwa mwili siku hii? Mbona mnasema kwamba kukosekana kwa ufunuo kutoka kwa Mungu kunathibitisha kwamba Hajakuwa mwili? Ni lazima Mungu amweleze mwanadamu kabla ya kuanza kazi Yake? Ni lazima apate idhini kutoka kwa mwanadamu? Isaya alitangaza tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini lakini hakutabiri kwamba Maria angejifungua Yesu. Mbona basi mlimwamini Yesu aliyezaliwa na Maria? Hakika imani yenu siyo isiyokuwa na uhakika na mkanganyiko! …

Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni mkondo sawa, na unastahili kuukubali bila wasiwasi wowote hata kidogo; hufai ya kuchukua na kuchagua kipi cha kukubali. Ukipata ufahamu zaidi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari zaidi Kwake, basi hili silo tendo lisilohitajika? Huna haja kutafuta uthibitisho zaidi kutoka kwa Biblia; iwapo ni ya Roho Mtakatifu huna budi kuikubali, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao tu ndio wanaoifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu kanuni na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa na uhakika juu ya hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale “watu werevu,” ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Bwana Yesu alisema, “Yesu akasema kwake, Tomaso, kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini.” Maneno haya yana maana kwamba alikuwa tayari ameshutumiwa na Bwana Yesu. Hili halihusu kubarikiwa ama kutobarikiwa. Ni kuhusu ukweli kwamba hutapokea kitu chochote usipoamini; ni kwa kuamini tu ndiyo utapokea. Je, una uwezo wa kukiamini chochote ikiwa Mungu ataonekana kwako binafsi tu, Akuruhusu umwone, na Akushawishi? Kama mwanadamu, una sifa gani za kumtaka Mungu aonekane kwako binafsi? Una sifa gani za kumfanya Mungu azungumze binafsi na mwanadamu mpotovu kama wewe? Aidha, ni nini kinachokufanya uwe na sifa za kumhitaji Mungu akueleze kila kitu wazi kabla ya wewe kuamini? Kama wewe ni mwenye busara, basi utaamini baada tu ya kusoma maneno haya ambayo Mungu amenena. Kama kweli una imani, basi haijalishi afanyacho Mungu au kile Asemacho. Badala yake, utakuwa na uhakika kamili kuwa kilisemwa na Mungu ama kilifanywa na Mungu punde uonapo kwamba maneno haya ni ukweli, na tayari utakuwa umejiandaa kumfuata mpaka mwisho. Hupaswi kushuku hili.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

“Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho.” Mmeyasikia sasa maneno ya Roho Mtakatifu? Maneno ya Mungu yamekuja juu yenu. Mnayasikia? Mungu anafanya kazi ya neno katika siku za mwisho, na maneno haya ni yale ya Roho Mtakatifu, kwani Mungu ni Roho Mtakatifu na Anaweza pia kuwa mwili; kwa hivyo, maneno ya Roho Mtakatifu, yalivyosemwa zamani, ni maneno ya Mungu mwenye mwili wa leo. Kuna wanadamu wajinga wanaoamini kwamba maneno ya Roho Mtakatifu yanapaswa kuja chini kutoka mbinguni hadi kwa masikio ya mwanadamu. Yeyote anayefikiria hivi hajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, matamshi yaliyosemwa na Roho Mtakatifu ni yale yaliyosemwa na Mungu aliyekuwa mwili. Roho Mtakatifu hawezi kuongea moja kwa moja na mwanadamu, na Yehova hakuongea moja kwa moja na watu, hata kwa Enzi ya Sheria. Si ungekuwa uwezekano wa chini zaidi kwamba Angefanya hivyo kwa enzi ya leo? Kwa Mungu kunena matamshi ili kutekeleza kazi, lazima Awe mwili, la sivyo kazi yake haiwezi kukamilisha malengo Yake. Wanaomkataa Mungu ni wale wasiojua Roho ama kanuni ambazo Mungu hufanya kazi. Wanaoamini kwamba sasa ni enzi ya Roho Mtakatifu lakini bado hawakubali kazi Yake mpya ni wale wanaoishi kwa imani isiyo dhahiri. Wanadamu kama hawa hawatapokea kamwe kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wanaotaka tu Roho Mtakatifu azungumze moja kwa moja na kutekeleza kazi Yake, lakini bado hawakubali maneno ama kazi ya Mungu mwenye mwili, kamwe hawataweza kuchukua hatua katika enzi mpya ama kupokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp