Wanawali wenye hekima ni nini? Wanawali wapumbavu ni nini?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Zamani, watu wengine walibashiri “mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu”. Ingawa utabiri huo si sahihi, lakini pia si wenye makosa kabisa—hivyo, Naweza kuwapa ninyi maelezo fulani. “Mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu” kwa pamoja hawawakilishi idadi ya watu wala aina ya mtu. “Mabikira watano wenye busara” inaashiria idadi ya watu, na “mabikira watano wapumbavu” inaashiria aina moja ya watu, lakini hakuna kati ya hivi viwili inayorejelea wana wazaliwa wa kwanza. Badala yake, vinawakilisha uumbaji. Hii ndiyo maana wameulizwa waandae mafuta katika siku za mwisho. (Viumbe hawana sifa Yangu; kama wanataka kuwa wale wenye busara, wanahitaji kuandaa mafuta, na hivyo wanahitaji kujitayarisha na maneno Yangu.) “Mabikira watano wenye busara” wanawakilisha wana Wangu na watu Wangu kati ya wanadamu Niliowaumba. Wanaitwa “mabikira” kwa sababu wanapatwa na Mimi, licha ya wao kuzaliwa duniani; mtu anaweza kuwaita watakatifu, kwa hivyo wanaitwa “mabikira.” “Watano” liliotajwa awali linawakilisha idadi ya wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewajaalia. “Mabikira watano wapumbavu” linarejelea watendaji huduma, kwa kuwa wananifanyia huduma bila kushikilia hata umuhimu mdogo kwa maisha, wakifuatilia tu mambo ya nje (kwa sababu hawana sifa Yangu, bila kujali kile wanachokifanya, hicho ni kitu cha nje), na hawawezi kuwa wasaidizi Wangu wenye uwezo, kwa hiyo wanaitwa “mabikira wapumbavu.” “Watano” lililotajwa awali linamwakilisha Shetani, na ukweli kwamba wanaitwa “mabikira” kunamaanisha wameshindwa na Mimi na wanaweza kunifanyia Mimi huduma—lakini watu kama hao sio watakatifu, kwa hivyo wanaitwa watendaji huduma.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 116

Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. … “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

Wale wote ambao huweza kutii matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa. Mungu anataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anataka wale ambao hukubali na kujua kazi Yake ya karibuni zaidi. Kwa nini husemwa kwamba lazima uwe mwanamwali safi? Mwanamwali safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, kuweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Wale “wanawali wenye hekima” ni wale ambao wanaweza kuijua sauti ya Mungu na kuitambua sauti ya “bwana harusi” na hivyo wanaweza kumkubali na kumtii Kristo, na hapokukaribishakukaribisha kurudi kwa Bwana na kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Kwa sababu “wanawali wapumbavu” hawaijui sauti ya “bwana harusi” na hawawezi kuitambua sauti ya Mungu, wanamkataa Kristo na kuendelea kumtamani sana Mungu asiye yakini mpaka wanapoachwa na kuondolewa na Mungu. Tunaweza kuona kwamba katika imani yetu, ni vigumu sana kumkubali Kristo bila imani ya kweli. Wale ambao wanakataa kumkubali Kristo wataikosa “sherehe ya harusi ya Mpendwa” na hawawezi kukubaliwa tena na Bwana nyumbani katika ufalme wa mbinguni na hawawezi kuingia katika sehemu ambayo Mungu amemwandalia mwanadamu. Hivyo, ikiwa watu wanaweza kumpokea Kristo wa siku za mwisho na kuitii kazi Yake ni sababu muhimu ya kuamua iwapo watu watafanikiwa au kutofanikiwa katika imani yao kwa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Bwana Yesu alitabiri katika Biblia kwamba wakati wa kurudi Kwake kutakuwa na aina mbili za watu—Aliwatumia mabikira wenye busara na mabikira wapumbavu kama mfano kwa waumini wote wa Enzi ya Neema: Wote wanaosikia sauti ya Mungu na wanaweza kuikubali na kuitii ni mabikira wenye busara; wote wasioweza kusikia sauti ya Mungu, wanaosikiliza lakini hawaamini na bado wanaikana, ni mabikira wapumbavu. Je, mabikira wapumbavu wanaweza kunyakuliwa? La, hawawezi. Kwa hiyo hawa mabikira wapumbavu na wenye busara wanaweza kufichuliwa vipi? Wanafichuliwa kupitia neno la Mungu, na kupitia mitazamo yao baada ya wao kusoma maneno ya Mungu katika siku za mwisho—Neno laonekana katika Mwili. Baada ya waumini wengine kuyasoma, wanasema, “Maneno ya kina kweli—maneno haya yana ukweli.” Baada ya wao kuyasoma tena kwa makini, wanasema, “Maneno haya hayawezi kuwa yametoka kwa mtu wa kawaida; yanaonekana kuwa yametoka kwa Mungu.” Kisha wanaangalia kwa makini tena na kusema, “Hii ni sauti ya Mungu; haiwezekani kwamba maneno haya yalitoka kwa mwanadamu!” Mtu huyu amebarikiwa; yeye ni bikira mwenye busara. Kuhusu mabikira wapumbavu, wengine ni wachungaji, wengine ni wazee, wengine ni wahubiri, na wengine ni waumini waliokanganywa wanaotaka tu kula hadi washibe. Mtazamo wao ni upi baada ya kusoma neno la Mungu? “Hmmm, maneno haya hayakubaliani na fikira na mawazo yangu, sikubaliani.” Na baada ya kuyasoma kwa makini tena, wanasema: “Baadhi ya maneno haya yanaonekana kuwa ya maana, lakini hilo haliwezekani; hii haiwezi kuwa kazi ya Mungu.” Kwa hiyo kwa mara nyingine tena, halikubaliani na fikira na mawazo yao. Mwishowe, kadiri wanavyolisoma, ndivyo linavyokubaliana na fikira zao kwa kiwango kidogo zaidi. Wanasema: “Hili silo neno la Mungu—siwezi kulikubali. Huyu ni bandia, Kristo wa uongo anayejaribu kuwadanganya watu. Siwezi kuliamini!” Huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni Mfarisayo, bikira mpumbavu. Wale ambao ni mabikira wenye busara na wale ambao ni mabikira wapumbavu wanafichuliwa na neno la Mungu. Ni neno la Mungu katika siku za mwisho linalowaainisha na kuwagawa katika makundi yao, na kisha Mungu ataanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Mabikira wenye busara wataisikiza sauti ya Bwana, hasa kwa sababu ni wale wanauopenda na kuutafuta ukweli. Wanatamani kuonekana kwa Mungu; hii ndiyo maana wanaweza kutafuta na kuchunguza kuja kwa Bwana, na ndiyo maana wanaweza kuitambua sauti ya Bwana. Kwa kuwa mabikira wapumbavu hawaupendi ukweli, hawatafuti au kuchunguza kuja kwa Bwana, wakijua tu kushikilia sheria kwa ukaidi. Wengine wao wanasisitiza kwamba hawatamkubali au kumchunguza Bwana yeyote Asiyekuja juu ya wingu. Wengine wanatii utawala wa hila wa wachungaji na wazee wa dunia ya dini kikamilifu. Chochote ambacho wachungaji na wazee wanasema, watasikiza na kufuata. Wanamwamini Bwana kwa jina, lakini kwa kweli, wanafuata na kuwatii wachungaji na wazee hawa. hawaichunguzi njia ya kweli kwa ajili yao wenyewe na hawawezi kuitambua sauti ya Bwana. Wengine hata ni wapumbavu zaidi. Kwa kuwa kuna Makristo wa uongo wanaoonekana katika siku za mwisho, hawamtafuti au kumchunguza Kristo wa kweli na hata wanaweza kumkana na kumshutumu. Je, huku si kukata pua ili uunge wajihi? Hili pia ni dhihirisho la bikira mpumbavu.

Kimetoholewa Kutoka Katika Majibu ya Mswada wa Filamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp